Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
JamiiForums imewasiliana na Mmiliki wa Kampuni ya Kiliki, Gabriel Kiliki ambaye gari lake ndilo lilihusika, amesema “Nimeelezwa Baba wa marehemu anataka fidia Dola 3,200 (Tsh. Milioni 8.2) kisha Juma ataachiwa, baada ya hapo kwa kuwa marehemu alikuwa na Wake watatu, kila mmoja wao aelezee mahitaji yao ya fidia, yakitimizwa wataachia gari pamoja na Juma atarusiwa kuondoka Sudani.”
Ameongeza “Hatujataka kufanya malipo hayo kwa kuwa awali kuna malipo tuliambiwa yanahitajika ili wamuachie, yalifanyika na haikujulikana yalipoteaje, Wakala wa Bima ya gari kule Sudani Kusini tunayemtumia anaitwa Alex, naye hatoi ushirikiano kwetu na hatujui nini kinaendelea.”
JamiiForums imewasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje, Mindi Kasiga ambaye awali alisema Idara ya Afrika inafuatilia suala hilo, ambapo pia alisema Tanzania haina Ubalozi Sudani Kusini, amesema “Nitakurudia kukupa mrejesho.”
Ilivyokuwa awali, soma hapa ~ Dereva Mtanzania anashikiliwa Sudan Kusini baada ya kugonga mtu, inadaiwa Polisi wagoma kumuachia wanataka hela