Dereva na konda wanusurika kichapo baada ya kuwanyima abiria raha ya Flyover

Dereva na konda wanusurika kichapo baada ya kuwanyima abiria raha ya Flyover

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,311
Reaction score
15,640
Juzi siku moja baada ya uzinduzi wa barabara ya juu kuna daladala ya kutokea Makumbusho kwenda Buguruni ilileta tafrani baada ya konda kumwambia dereva asipite flyover ili ajazie abiria pale kituo cha mafuta cha Oilcom iliyo pembeni ya flyover.

Dereva kama kawaida yao wanatumiaga akili za konda kuendesha gari nae akapita chini wakati abiria walikua wanahamu kupita juu maana wengi walikua hawajaizindua bado na hawakupenda kitendo hicho cha utovu wa nidhamu cha kuwanyima uroda wa flyover wakaanza kurusha maneno.

Kilichowauma abiria zaidi ni baada ya konda kukosa abiria pale sheli ndipo wakataharuki kulikua na sababu gani kuwanyima raha. Mzozo ulikua mkubwa mpaka daladala ikapark pembeni na kondakta kukunjwa shati huku dereva akisema yeye alimsikiliza konda ila nae alitamani kupita juu.

Kondakta huyo ilibidi awe mpole baada ya kuona gari zima limechachamaa na kulazimika kuomba radhi na kukiri hadharani kwamba hatorudia tena kufanya upuuzi wa aina hiyo na ndipo safari ikaendelea huku abiria wakiangalia kwa uchungu jinsi magari mengine yanavyopita juu ya flyover wakati wao wamenyimwa hiyo raha.
 
Ujinga ujinga tu[emoji3][emoji3]
Eti raha ya flyover, na hii nayo unakula buku 7 sio?
Tulia we wa mkoani unaewaza siasa muda wote wakati wenzio tunawaza mishe
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Mishe za kulilia kupita darajan? Ebu kuwa serious mkuu..
Wenzio wametoka mishe choka mbaya wanataftia kwa kutolea stress halafu konda ajichanganye unategemea nini... Dar hujaijua vizuri jamaa
 
Hao itakuwa ni CHADEMA wanapinga na bado wanatamani kupita
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Japokuwa sijamuamini mtoa mada lakini nimecheka sana 😂😂😂
 
Oil com pana kituo toka lini? We kubali tu kwamba hii story umetumga...

Vipi wewe ndo ulimkunja konda?
Though sio kituo rasmi ila daladala zinatoka mawasiliano zinashusha na kupakia sana pale oilcom karibu na Mataa...ungekua unapanda daladala hili wala sio jambo jipya...
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Though sio kituo rasmi ila daladala zinatoka mawasiliano zinashusha na kupakia sana pale oilcom karibu na Mataa...ungekua unapanda daladala hili wala sio jambo jipya...
Muache mkuu huyu jamaa anajiaibisha tu
 
Back
Top Bottom