Dereva na konda wanusurika kichapo baada ya kuwanyima abiria raha ya Flyover

Dereva na konda wanusurika kichapo baada ya kuwanyima abiria raha ya Flyover

Mimi ndio sijaelewa au mleta uzi amedanganya. Kwanijuavyo, ukipita barabara ya chini kabisa, hauwezi kumuona aliyepita juu kule kuelekea riverside. Hao abiria waliokuwa wakiwatazama wengzao kwa uchungu kule juu wana shingo size gani
 
Hamna kitu hapa zaidi ya chai, we lamba buku Saba yako sepa
 
Ujinga ujinga tu[emoji3][emoji3]
Eti raha ya flyover, na hii nayo unakula buku 7 sio?
Uzi mzuri kwenu ni ule wa kumsifia kibaraka nyingine zote mtaziita buku Saba au hazina maana
 
...

Dereva kama kawaida yao wanatumiaga akili za konda kuendesha gari nae akapita chini wakati abiria walikua wanaham kupita juu maana wengi walikua hawajaizindua bado na hawakupenda kitendo hicho cha utovu wa nidhamu cha kuwanyima uroda wa flyover wakaanza kurusha maneno...
Neno URODA limetumika lisipostahili.
 
Banamume ba dar balilia flyover ati balitaka kupita juu bagapitishwa chini bagalalamika kiasi cha kumutowa roho kondakita.
 
Wana Dar wanataka angalau waonje matumizi ya kodi yao, maana si kwa ukapa huu!
 
Ndipo safari ikaendelea huku abiria wakiangalia kwa uchungu jinsi magari mengine yanavyopita juu ya flyover wakati wao wamenyimwa hiyo raha.

Hii ndio pekee iliyonivutia sana pia inafurahisha.
 
Juzi siku moja baada ya uzinduzi wa barabara ya juu kuna daladala ya kutokea Makumbusho kwenda Buguruni ilileta tafrani baada ya konda kumwambia dereva asipite flyover ili ajazie abiria pale kituo cha mafuta cha Oilcom iliyo pembeni ya flyover.

Dereva kama kawaida yao wanatumiaga akili za konda kuendesha gari nae akapita chini wakati abiria walikua wanahamu kupita juu maana wengi walikua hawajaizindua bado na hawakupenda kitendo hicho cha utovu wa nidhamu cha kuwanyima uroda wa flyover wakaanza kurusha maneno.

Kilichowauma abiria zaidi ni baada ya konda kukosa abiria pale sheli ndipo wakataharuki kulikua na sababu gani kuwanyima raha. Mzozo ulikua mkubwa mpaka daladala ikapark pembeni na kondakta kukunjwa shati huku dereva akisema yeye alimsikiliza konda ila nae alitamani kupita juu.

Kondakta huyo ilibidi awe mpole baada ya kuona gari zima limechachamaa na kulazimika kuomba radhi na kukiri hadharani kwamba hatorudia tena kufanya upuuzi wa aina hiyo na ndipo safari ikaendelea huku abiria wakiangalia kwa uchungu jinsi magari mengine yanavyopita juu ya flyover wakati wao wamenyimwa hiyo raha.
Mgombea wetu wa CCM akiwa Zanzibar anawaeleza Wazanzibar kuwa wasiondoke uwanjani hapo maana akimaliza hotuba bado Kuna show kabambe kutoka kwa wasanii na watamuona nae akicheza.... Wazenji nao viburi wakaondoka wakati anazungumza. Aisee!
 
Oil com pana kituo toka lini? Wewe kubali tu kwamba hii story umetunga...

Vipi wewe ndio ulimkunja konda?
Mkuu pale hakuna kituo ila ni dark bus stop kwa wale wanaopata shida kwenda simu.
 
Back
Top Bottom