Dereva wa lori auwawa na mlinzi wa puma petrol station Morogoro


Mlinzi amekosa Ilmu...hasira hasara
 
Siungi mkono mauaji ila sidhani kama Kuna watu wanadharau kama ma driver na ni wa magari yote labda wanazidiwa na makatibu waenezi wa chama kijani kutoka venezuela
 
Inasikitisha sana mlinzi anaua Dereva kisa elfu 15 ya parking? Mental illness is real ,migambo wawe wanapewa virungu tu wakiwa kwenye malindo maana hao watu wanalipwa laki na nusu kwa mwezi hivyo wanakuwa na stress sana.
Huwezi kulinda Petrol station kwa Rungu Wazee wa KAZI wanakuja kubeba Hela mapema tu..
 
Muislam amemuua ndugu yake Muislam! subhanallah, tena ametoka msikitini kuswali swalaatil fajr maskini. Kuna watu imani hawana, huruma hawana, wanatanguliza maslahi mbele, na yote ni mambo ya dunia, yupo tayari kuuwa kisa tu 500/=

ayat 33 from Surah Al-Isra



Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa.

Wala msiuwe nafsi yoyote ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa ila kuuwa huko kukiwa kwa haki, kwa kuwa nafsi hiyo inastahiki kuuwawa kwa ajili ya kisasi au kuwa ni adhabu ya sharia. Na mwenye kuuliwa kwa kudhulumiwa Sisi tumempa jamaa yake wa karibu haki juu ya yule muuwaji, kwa kutaka kwa Qadhi auliwe kwa kisasi. Lakini naye asipite mpaka katika kuuwa, akataka kumuuwa mtu mwengine asiye kuwa muuwaji, au kwa kuwauwa wawili badala ya mmoja. Kwani Mwenyezi Mungu amemsaidia huyo kwa kumpa haki ya kisasi au kulipwa fidiya. Basi haimfalii kukiuka mipaka iliyo wekwa.
 
Nchi ngumu hii kils mtu kapagawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…