Dereva wa SATCO aoneshewa bastola, abiria wamnusuru "walitaka kumchukua"

Tukio la kushangaza limetokea katika eneo la Makole, baada ya dereva wa basi la kampuni ya SATCO lenye namba za usajili T308 EME kudaiwa kutishiwa kwa silaha ya moto na mtu ambaye hakufahamika, aliyekuwa akiendesha gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T881 ENZ.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa basi hilo lilikuwa likitoka katika stendi ya mabasi jijini Dodoma kuelekea mkoani Geita, ambapo lilipofika eneo la Makole, dereva wa Land Cruiser alidaiwa kulipita basi hilo kwa upande, hali iliyosababisha magari hayo kugongana.

Baada ya tukio hilo, mashuhuda wanadai kuwa dereva wa Land Cruiser alishuka akiwa na silaha ya moto inayodaiwa kuwa ni bastola na kumfuata dereva wa basi, akimtaka ashuke kwenye basi hilo na kuingia katika gari aina ya Land Cruiser.

Tukio hilo limezua hofu miongoni mwa Wananchi waliokuwa eneo hilo, huku baadhi yao wakilaani tukio hilo na kuitaka Serikali pamoja na vyombo vya usalama kuchukua hatua za haraka ili kubaini ukweli wa tukio hilo na kuwachukulia hatua wahusika endapo madai hayo yatathibitishwa.

Hata hivyo mara baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuchukua magari yaliyohusishwa (basi na land cruiser) kwa ajili ya uchunguzi.
ok. :1Head:
 
Hii nchi siku hizi kila ninayemuona yuko juu ya sheria. Kasoro mimi tu.
Hili siyo la kushangaza. Rais anaendesha nchi kihuni wlio chini yake unadhani watafanya nini? Polisi imegeuka kitendo cha uongo na uhuni. Ila wananchi wanachoniacha hoi ni hiyo sentensi ambayo kila mtanzania ameikariri hata ukimwasha usingizini anaisema ''tunaomba serikali iliangalie hili jambo''. Yaani ''nyani'' hawaoni kabisa uhusiano wa huu uhuni na serikali.
 
Landcruizer namba ENZ bado jipya sana,ukute alichukulia mkopo na colateral kaweka nyumba yake ya kuishi,kama chuma kiko mfukoni inahitaji moyo sana usikitoe...
Kwanini alikiwa anamwita waingie garini? Na kwanini kaoiga simu limekuja cruiser jingine kama hilo? Hujiongezi tu kuwa hayo sio ya watu binafsi?
 
Tukio la kushangaza limetokea katika eneo la Makole, baada ya dereva wa basi la kampuni ya SATCO lenye namba za usajili T308 EME kudaiwa kutishiwa kwa silaha ya moto na mtu ambaye hakufahamika, aliyekuwa akiendesha gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T881 ENZ.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa basi hilo lilikuwa likitoka katika stendi ya mabasi jijini Dodoma kuelekea mkoani Geita, ambapo lilipofika eneo la Makole, dereva wa Land Cruiser alidaiwa kulipita basi hilo kwa upande, hali iliyosababisha magari hayo kugongana.

Baada ya tukio hilo, mashuhuda wanadai kuwa dereva wa Land Cruiser alishuka akiwa na silaha ya moto inayodaiwa kuwa ni bastola na kumfuata dereva wa basi, akimtaka ashuke kwenye basi hilo na kuingia katika gari aina ya Land Cruiser.

Tukio hilo limezua hofu miongoni mwa Wananchi waliokuwa eneo hilo, huku baadhi yao wakilaani tukio hilo na kuitaka Serikali pamoja na vyombo vya usalama kuchukua hatua za haraka ili kubaini ukweli wa tukio hilo na kuwachukulia hatua wahusika endapo madai hayo yatathibitishwa.

Hata hivyo mara baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuchukua magari yaliyohusishwa (basi na land cruiser) kwa ajili ya uchunguzi.
Tanzania chini ya hawa watu wanne 1. Rais SAMIA, CDF MKUNDA na IGP WAMBURA , DGTIS MOMBO hatuko salama na nchi si salama kwa wananchi na mali zao hawa viongozi pamoja na vyombo vya ulinzi hawajali usalama na uhai wa raia.
 
Tukio la kushangaza limetokea katika eneo la Makole, baada ya dereva wa basi la kampuni ya SATCO lenye namba za usajili T308 EME kudaiwa kutishiwa kwa silaha ya moto na mtu ambaye hakufahamika, aliyekuwa akiendesha gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T881 ENZ.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa basi hilo lilikuwa likitoka katika stendi ya mabasi jijini Dodoma kuelekea mkoani Geita, ambapo lilipofika eneo la Makole, dereva wa Land Cruiser alidaiwa kulipita basi hilo kwa upande, hali iliyosababisha magari hayo kugongana.

Baada ya tukio hilo, mashuhuda wanadai kuwa dereva wa Land Cruiser alishuka akiwa na silaha ya moto inayodaiwa kuwa ni bastola na kumfuata dereva wa basi, akimtaka ashuke kwenye basi hilo na kuingia katika gari aina ya Land Cruiser.

Tukio hilo limezua hofu miongoni mwa Wananchi waliokuwa eneo hilo, huku baadhi yao wakilaani tukio hilo na kuitaka Serikali pamoja na vyombo vya usalama kuchukua hatua za haraka ili kubaini ukweli wa tukio hilo na kuwachukulia hatua wahusika endapo madai hayo yatathibitishwa.

Hata hivyo mara baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuchukua magari yaliyohusishwa (basi na land cruiser) kwa ajili ya uchunguzi.
Tanganyika imekuwa hovyo kabisa
 
Naam, kila siku nasema njia ya kumaliza utekaji ni raia kuanza kumiliki silaha wenyewe ili mtekaji akitoa silaha na wao wanatoa .

Tofauti na hapo ni mobilization kama hapo wananchi walivyojaa na kumuweka mwenye silaha katika mazingira hatarishi hata silaha yake kuonekana haina msaada.
 
.
 
Attachments

  • IMG-20260921-WA0024.jpg
    IMG-20260921-WA0024.jpg
    128.9 KB · Views: 9
Back
Top Bottom