Dereva wangu kaua kakimbia

Dereva wangu kaua kakimbia

Gari yangu nitaipataje pale? Maana wanataka hela...

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Kubali kwenda mahakamani, lkn jiaandae kutaja alipo dereva wako. Ukishindwa kutaja kesi unayo lkn si ya usalama
 
Una elimu gani? Hujawahi kusikia tajiri anawajibishwa kwa kosa la mfanyakazi? Ili akwepe kesi shart amlete dereva kwani huwezi ajiri usiyemjua

How many years I spent in classes got nothing to do with what I know and life experince, I gave him my experience. And no body can be accused of something he/she didn't do, believe that. Only ignorant people can bend to that, and the police do that it doesn't mean they are right, they are wrong and if u stand up to them, u ---- them off
 
Mahakama is a neutral ground, hujafanya kosa lolote na hutakiwi kuogopa. Ni driver wako na ulimpa gari likiwa halina tatizo na yeye ana sifa zote za kuliendesha, u are done. Sio kazi yako kumtafuta kama ametoroka, ni kazi ya police
 
Alipe faini ya nini tena mkuu?
Kama wamekupeleka mahakamani that's okay, you didn't comment the offense and you are responsble ndio maana ulikwenda police kujua tatizo. Utalipa fine kawaida ili warelease the vehicle na ukiamua kunyooka na police unaweza kwa sababu hawakuwa na sababu kukuweka lock up
 
Alipe faini ya nini tena mkuu?

Itategemea na set up ya case, makosa yote ya barabarani ambayo yamesababishwa na uzembe wa upande fulani yana fine mkubwa. Huyo ameua, for example, hawezi rudisha uhai wa mtu ila mahakama itamcharge gharama kulingana na uzembe utakaobainika kufanyika kabla na wakati wa tukio
 
Kaka kuna acts ambazo an employer anakualiable kwa acts za employee wake..hii kisheria inaitwa vicarious liable..liability yako itakuja iwapo kuna vitu ulikua na uwezo wa kuvicontrol dereva wako asivifanye kabla ya kupata ajali..mfano, kuhakikisha dereva wako yuko sobber b4 ya safari ama gari iko in a gud condition tairi ziko poa na kila kitu,kuhusu kufungwa..somthng lyk false imprisonment inaweza kuaply bt rely kwa writ ya herbius corpus...

hapa si fesibuku mkuu
andika kama GT!!
 
RUSHWA ANDIO mpango mzima___
shikamoo ccm
 
Tarehe 31 december asubui derevva wangu aligonga mtu akafari pale pale na hakusimama na kakimbia na kuterekeza gari, polisi wameichukua gari, na kesi ipo mahakamani, sasa me mmiliki wa gari niliifuata gari wakaniweka rock up mpaka Dereva apatikane nimekaa siku mbili...sijajua kwa nini walinikamata na kuniweka ndani wakati me sijapatisha ajali na sikuwepo hapo? maana sasa kesi inapelekwa mahakamani na sijajua nitajibu nini kule na ni mara yangu ya kwanza kusimama mahakamani

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Swali lililo wazi ...je police wanataarifa gani kama aliyegonga si wewe na ni dereva wako?na mmiliki wa gari niwewe. Jengine ni kitu cha kawaida unavyofanya uajiri hata kama ni shamba boy or house kuna vitu vya kuzingatia ikiwemo hilo la kupata udhamini,yaani mtu ambae atamdhamini mtu uliyemuajiri na kupata taarifa stahiki juu ya mtu unaemwajiri.na hata hati ya maandiko kuonesha umemwajiri flan bin flan from sehem flan na mdhamini wake moja na mbili hawa hapa,hili litakusaidia pindi itokeapo kesi kama hii
 
huyo dereva una mkataba naye na wadhamini 2 kama una mkataba naye na wadhamini wawili hakuna shida kama huna inakula kwako unachukua dereva kideiwaka deiwaka .
 
Una elimu gani? Hujawahi kusikia tajiri anawajibishwa kwa kosa la mfanyakazi? Ili akwepe kesi shart amlete dereva kwani huwezi ajiri usiyemjua

Hiyo inakuwa kwenye madai " tort" ila kwa mujibu wa facts as presented, hakuna kesi ya jinai anayoweza kushitakiwa nayo. Ila wafiwa wanaweza kufungua kesi ya madai ikimuunganisha dereva, mmiliki na kampuni ya insurance.
 
Mambo muhimu ya kuzingatia ili kuthibitisha kuwa si wewe mwenyewe uliyekua unaendesha ni pamoja na;

1 Mkataba wa maandishi baina yako , dereva na wadhamini wake.
2 Nakala ya leseni ya dereva kuthibitisha uhalali wake wa kuendesha chombo cha moto kilichosababisha ajali
3 Mashuhuda wa ajali yaweza kuwa watembea kwa mguu au abiria waliokuemo ndani ya gari iliyopata ajali.
Mengineyo
1 Road worthiness ya gari
2 Road license
3 Bima

Wewe ulikamatwa ili uisaidie polisi kiupelelezi na kwa usalama wako dhidi ya hasira za wafiwa

Polisii kazi yao ni kukamata makosa na kupeleka mahakamani (kama kunguru akamatavyo kifaranga wa kuku akikosa huchukua hata nyasi) mambo mengine ni uTZ tu nenda nayo mporampora .
 
Back
Top Bottom