Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mji wa Derna mashariki ya Libya ni mji wenye historia kubwa katika nchi hiyo.Ndiko walikozikwa maswahaba wengi wa Mtume s.a.w nchini humo jumla yao wakifikia 70.Na hata jeshi la Amru ibn Aas liliingia mji huo mwanzo kabla kuendelea upande wa magharibi.
Katika historia yake uliwahi kupigana na jeshi la Marekani na ndiko Marekani ilikopata ushindi wake wa mwanzo nje ya nchi yake mwaka 1805.
Ni mji uliotoa wapiganaji wengi waliokwenda kupigana nchini Iraq na Afghanistani.Baadae mji huo ulikuwa ni mji wenye uhasama sana na Muammara Ghadafi na ni miongoni mwa miji ya mwanzo ilioanzisha uasi dhidi yake.
Machafuko nchini Libya yaliyoungwa mkono na mataifa ya magharibi yalipofanikiwa kumuondoa Ghadafi madarakani kwa kumuua ,mji huo uliamua kujitenga na kujitawala kiislamu tangu mwaka 2011.Wezi walikatwa mikono na wazinifu kupigwa viboko.Msikiti uliotumika kama kituo cha utawala ni ule unaoitwa masjidu swahabi ambao ndio uko karibu na makaburi ya maswahaba waliozikwa mjini hapo
Hata hivyo wakazi wa mji huo walilalamika na kupeleleka malalamiko yao mpaka UN ambapo vikundi vingi vya wanaharakati vilingia kutetea wale waliopinga sharia.Wengi wa wapinzani hao walihama mji huo kukimbia utawala wa sharia.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipelekea mji huo kupigwa sana na generali Haftar ambaye alikuwa upande wa wanaopinga utawala wa kiislamu.Kauli zake za kupambana na vikundi vya kigaidi vilimpatia jenerali huyo misaada mingi ya kijeshi kutoka nje..Hatimae alifanikiwa kuwaondoa watawala hao.Na japo alifanikiwa kwa hilo lakini amebaki kutowaamini wakazi wa mji huo kutokana na hisroria yake,kama kwamba watafufuka wampinge.Kutokana na hilo Generali Haftari huwa ana mshirika wake anayetawala kwa sera zake bila mwenyewe kufika.
Katika miaka michache iliyopita historia ya mji huo imebadilika.Mbali na kuwa mji wa anasa pia ni miongoni mwa miji yenye upenzi mkubwa na mpira wa miguu..Timu ya 4 kwa ukubwa nchini Libya imo mjini Derna pamoja na uwanja mkubwa wa mpira.Kutwa kucha wakazi wengi wa mji huo wanajadili mpira na kubeti.Baadhi ya wachezaji wake maarufu ni akina Abdulhaq Al Tashani, Ahmed Souleimen Neffati, Idris Mikraz na Anis Mikraz.chini ya timu ya Darnes
Mafuriko yaliyotokea juzi yanakisiwa kusomba majumba mengi sana na wakazi wake wanaokadiriwa 20,000 kuwapeleka baharini ama kukandamizwa chini ya majengo yaliyoporomoka kutokana na mvua kali iliyonyesha kwa siku kadhaa.Mvua hizo zilizotokana na kimbunga chenye jina linalofanana na mji huo kilichoitwa Daniel .Mvua zilisababisha mabwawa mawili makubwa milimani kuzunguka mji wa Derna kujaa na kubomoka watu wakiwa wamelala.
Katika vipimo vya hali za hewa mvua iliyonyesha ina ukubwa wa sentimita 16 tu.Hata hivyo majengo yenye urefu mpaka ghorofa saba yamezama na kubomoka na hatimae kusombwa kuelekea baharini pamoja na wote waliokuwemo kama alivyoshuhudia Amna Al Ameen Absais,.
Masjid swahab pamoja na maji kupita eneo hilo na kusababisha uharibifu kwa majengo ya nje lakini bado umebaki katika hali nzuri.Kati ya maeneo yaliyoharibiwa vibaya ni pamoja na uwanja wa mpira wa Darne stadium.Wachezaji wanne maarufu wa Darne club ni miongoni mwa waliokufa katika janga hilo.