Deus Kibamba: Maendeleo endelevu yatapatikana kwa kupunguza maslahi ya viongozi wa kisiasa

Deus Kibamba: Maendeleo endelevu yatapatikana kwa kupunguza maslahi ya viongozi wa kisiasa

Mchambuzi wa masuala ya siasa nchini, Deus Kibamba, ameshauri kuwa ili nchi ipate maendeleo endelevu, ni muhimu kupunguza maslahi na stahiki mbalimbali wanazopata viongozi wa kisiasa, ambazo zimekuwa kubwa sana ikilinganishwa na stahiki za watumishi wa taaluma mbalimbali.

Kibamba ameongeza kuwa hali hii imesababisha watu wengi kuacha taaluma zao na kujiingiza katika siasa kwa lengo la kupata maslahi hayo makubwa, jambo ambalo linaathiri ukuaji wa sekta za taaluma na uchumi kwa ujumla.

Kibamba ametoa maoni haya leo, Julai 10, 2025, katika kipindi cha Mada Kuu cha TBC1 kilichojadili mada ya: “Kunani Bungeni.”

Natamani ningepewa kitengo cha kupanga mishahara... Maslahi.


This life is funny at all.
 
Yuko sahihi,kwasababu siasa ni ajira,ajira ambayo mwajiriwa anajipangia maslahi yake mwenyewe.Mwajiriwa ambaye kajipa utukufu,mamlaka na usimamizi wa waajiriwa wengine wote yeye ndiye awe kiongozi wao.Siasa ingekua ni huduma tusingekua tunaona yote hayo anayotokea.Tiba ya ilo nikupatikana katiba bora itakayobadilisha baadhi ya mambo ili maslahi yao yaendane na wajibu.
 
Kwanza niseme naumizwa mno na hali ya Taifa letu na nasikitishwa na Fikra zilizojaa kwa wengi wetu mkosoaji ndie Adui mkubwa na mzembe mlalaji bungeni ndio Tajiri na mwenye hali nzuri ya kimaisha.

NB:Siku zote Sehemu ambayo wajinga ni wengi kuliko wenye fikra pana maendeleo ni maneno tu na vijembe na sera za kujipatia kura za wajinga wa Taifa hilo.

Hivyo basi nasikitika sana juu ya Taifa langu la Tanzania daima kwa kuwa kuna mifumo ambayo bila kuwepo na viongozi wenye maamuzi magumu kwa ajili ya Taifa hilo basi majuto na ugumu wa maisha ndio style kubwa ya watoto wa Taifa hilo.

Tanzania bado tupo kwenye dimbwi la ukoloni mamboleo tunawekewa fikra za kutofikiria nje ya box tunaishi kinyonge mno kwa kuwa kila mmoja wetu anapambania kula kwake na sio Taifa lake.

Tumekosa imani za dini na mila zetu na tumekosa uzalendo wa Taifa letu hivyo hayo ndio matokeo ya mifumo yetu.
 
Kila mtu anakimbilia huku kufata ulaji....

Ova
 
Back
Top Bottom