GE2025 Deus Kibamba: Unono na mfumo wa sheria/katiba ni sababu inayowavutia wengi kuwania ubunge

GE2025 Deus Kibamba: Unono na mfumo wa sheria/katiba ni sababu inayowavutia wengi kuwania ubunge

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Wakuu
Kumekuwepo maswali mengi kuhusu wingi wa waliojitikeza kuchukua fomu za kutia nia na ubunge na udiwani, kupitia Kipindi cha Mada Kuu - TBC kilichofanyika Julai 10, 2025 Mchambuzi wa Masuala ya Siasa, Deus Kibamba alieleza badhi ya sababu zinazowavutia wengi kuwania nafasi ya Ubunge nchini
  1. Unono wa ubunge
Ameeleza kuwa Mbunge ana mshahara, posho maalum, posho ya vikao, bima daraja la kwanza, mafuta ya kutembelea ya gari, anakopeshwa gari italipwa kwa masharti madogo na mazuri, ana pasi ya diplomasia

2. Mfumo wetu wa Siasa

Mfumo wetu wa siasa, mfumo wa uchaguzi, unaweka kwamba lolote watakalotaka wanajipa wenyewe na siyo kwamba watapewa, kwa sababu wao ndiyo wanaohusika kutunga sheria, ambapo wakitaka sheria ya kuongeza maslahi ya wabunge wanaweza wakatunga
Hii ni tofauti na nchi zingine ambapo kunakuwa na chombo maalum linalosimamia Maslahi ya wabunge na maamuzi hufanywa na wananchi, ambapo ni tofauti kabisa na katiba au sheria ya nchi yetu

Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025



 
Back
Top Bottom