Deus Sangu ashiriki Mkutano wa Ahmadiyya, asema “Amani na uvumilivu ni msingi mkuu wa utekelezaji wa Dira ya 2050”

Deus Sangu ashiriki Mkutano wa Ahmadiyya, asema “Amani na uvumilivu ni msingi mkuu wa utekelezaji wa Dira ya 2050”

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
379
Reaction score
1,412
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Clement Sangu ameipongeza Jumuiya ya Ahmadiyya Tanzania kwa kuandaa Mkutano Mkuu (Jalsa Salana) wa 55 wa Mwaka 2026, huku akisisitiza umuhimu wa amani, upendo na mshikamano nchini.

Waziri Sangu ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba katika mkutano huo wa siku tatu uliofanyika Septemba 25 hadi 27, 2026, eneo la Ahmadiyya lililopo Kitonga, Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, amesema:

“Mkutano huu umejikita katika dhana ya kuondoa chuki na kuzidisha upendo katika Jamii ya Watanzania, hasa kutokana na Kauli Mbiu yao ya Mwaka huu ambayo nimeipenda ni ‘Upendo wa Watu Wote Bila Chuki kwa Yeyote’, hiyo inatuonesha kuwa Watanzania tuwe na upendo na kuachana na chuki,” amesema Waziri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) Mhe. Deus Clement Sangu amewas...webp

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) Mhe. Deus Clement Sangu amewas...webp
Amepongeza pia Jumuiya hiyo kuwakusanya takribani Watu 6000 kutoka maeneo tofauti na nchi tofauti wakiwemo Wajumbe na viongozi kutoka nchi za Ghana, Sierra Leone n.k

Amesisitiza kuwa ingawa Katiba inaeleza kuwa serikali haina dini, serikali inaziheshimu na kushirikiana na taasisi zote za dini nchini, na kwamba amani na uvumilivu ndio msingi mkuu wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2050.

Sheikh Khawaja Muzaffar Ahmad wa Tanzania
Upande wake, Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania, Sheikh Khawaja Muzaffar Ahmad, aliishukuru Serikali kwa kushiriki katika mkutano huo, akisema uwepo wa viongozi wa Serikali unaakisi mahusiano mazuri kati ya Serikali na jamii. Aliahidi kuendeleza ushirikiano huo na kuendelea kutekeleza malengo ya Jumuiya kwa manufaa ya jamii na Taifa.
DSC_5978.JPG

Musa Mewa wa Sierra Leone
Mjumbe kutoka Sierra Leone, Musa Mewa ambaye ni mmoja a washiriki wa mkutano huo, akibainisha kuwa hii ni mara yake ya pili kutembelea Tanzania na mara ya kwanza kuhudhuria mkutano huu wa kitaifa amesema tukio hilo linalenga kuwakumbusha watu kuhusu Umoja wa Mwenyezi Mungu (Tawheed), kuimarisha udugu wa kibadamu, na kutoa elimu na mafundisho ya dini.

Ameelezea umuhimu wa kumcha Mungu (Taqwa) kwa kuwa hiyo hali inasaidia kutotenda dhambi, kutomchukia jirani yake hata kama ni muumini wa Dini nyingine na anakuwa tayari kusaidia ubinadamu wote bila kujali imani zao.
Mohammed bin Salih wa Ghana
Amir na Mkuu wa Misioni wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini Ghana, Mohammed bin Salih ameeleza kufurahishwa kwake na ukuaji na ukomavu wa Jumuiya ya Ahmadiyya nchini Tanzania wakati wa Mkutano Mkuu (Jalsa Salana).

Amebainisha kuwa hiyo ni mara yake ya pili kutembelea Tanzania na kuhudhuria Jalsa Salana, ameeleza kuwa kuna hatua kubwa za maendeleo zilizopigwa na Jumuiya ya Ahmadiyya Tanzania katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, na kwamba sasa imekomaa na inaweza kulingana na jumuiya kongwe.

Profesa Dkt. Syed Basharat Ahmad
Prof. Dkt. Syed Basharat Ahmad, mwanasayansi na mtafiti kutoka Ujerumani (mwenye asili ya Kashmir, India), amesema hiyo ni mara yake ya kwanza kutembelea nchi za Afrika Mashariki.

Amesema Jalsa Salana ni fursa ya kuimarisha imani, kuongeza elimu, na kukumbushwa mafundisho ya kweli ya Uislamu na Qur'ani Tukufu kupitia hotuba mbalimbali, ikiwemo mada za ucha Mungu na usawa.

Ameeleza kuwa changamoto kubwa Duniani kwa sasa ni tamaa ya mataifa na watu wenye nguvu kutaka kuwakandamiza au kuwanyonya wanyonge na kwamba amani ya kweli itapatikana pale tu Wanadamu watakapojenga uhusiano wa dhati na Mwenyezi Mungu na kuwa na hofu ya Mungu.
photo_2026-09-28_08-32-10.jpg

Dkt. Mujeeb Salaam (PhD)
Dkt. Mujeeb Salaam (PhD) ambaye ni Mwanachama wa Ahmadiyya kutoka Nigeria ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kiislamu nchini Uganda (Islamic University in Uganda) amesema mkutano huo umekuwa fursa ya uamsho wa kiroho, kumkaribia Mungu, kuongeza imani, na kumfanya ajivunie kuwa Muislamu wa Ahmadiyya.
 
Back
Top Bottom