Dewji kulipa mishahara ya wachezaji Simba

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Mfanyabiashara maarufu nchini ambaye anashika nafasi ya 21 ya utajiri Afrika, Mohamed Dewji ameanza kulipa mishahara ya wachezaji wa klabu hiyo kutokana na klabu kutokuwa na mdhamini.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba zinasema kuwa pamoja na kulipa mishahara ya wachezaji Dewji amekubali pia kuendelea kuisaidia klabu hiyo kwa kutoa gharama za uendeshaji mpaka pale kipindi cha mpito cha miezi sita kitakapomalizika.

Sambamba na msaada huo anaoutoa kwa klabu yake ya samba Dewji aliyeomba kununua asilimia 51 ya hisa za Simba kwa shilingi bilioni 20 ameanza pia kutekeleza ahadi zake alizoahidi wakati ambapo Simba inaelekea katika mfumo wa mabadiliko ya kiuendeshaji.

Wakati mchakato wa kuiondoa samba kutoka katika mfumo wa sasa na kuiingiza katika mfumo wa hisa tayari Dewji amekubali kulipia nyasi za bandia zitakazoletwa nchini kwa aya ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa simba.

Itakumbukwa klabu hii imekuwa ikijiendesha yenyewe kupitia wanachama wake na sasa inatarajia kuhamia katika mfumo wa uendeshaji kupitia uuzaji wa hisa ambapo mwenyekiti wake huyo tayari ameomba kununua asilimia 51 ya hisa za klabu hiyo.
 
Si mlisema nyasi zipo bandalini nyie
Hela at okwi ilinunua toka Thailand MO anatoa hela ya ushuru n kodi za serikali mzigo utoke bandarini.

Vipi nyie geza ulole huko?
 
Unajua hujaeleweka?
 
Mchezaji mwenye mshahara mkubwa Simba analipwa 800,000 kwa hiyo naomba Simba wanipe total nxima ya mishahara ya Wachezaji niwe nawalipa Mimi.
 
Mchezaji mwenye mshahara mkubwa Simba analipwa 800,000 kwa hiyo naomba Simba wanipe total nxima ya mishahara ya Wachezaji niwe nawalipa Mimi.
Umeshindwa kumtumia pesa ya kumtibu mama yako jicho mishahara ya Simba utaiweza au kujishebedua tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…