DHAHABU na Mafuta ya Mawese yanatafutwa

Hahahaa, Mkuu wala siwezi kukuambia kwa sasa.

Wewe ongea na hao jamaa na utajilipa hukohuko kwao. Kama kuna tani kibao zinaingia, utapata tu na wewe chenji yako maana wakikukatalia, sisi huku tutawafungia BOMBA, hahahaaa.......

Wanasema usinunue mbeleko wakati hajazaliwa. Tufanye kwanza kazi na hayo mengine yatajileta tu.
Mkuu ngoja niwasiliane na wafanyabiashara wa mawese kigoma tuone kama wanaweza kupata hizo tone za wese kwa mwezi,je commision yangu ni % ngapi tukifanikisha hyo dili?
 
Mgombezi, sijui umetuma kwa jina gani.

Hebu angalia tena email yangu kama umeipatia maana hadi sasa nimejibu EMAIL zote ambazo nimeshazipata.

Kila ujumbe najitahidi kuujibu kutokana na habari ambayo hadi sasa ninayo.

Kuna ujumbe niliujibu leo asubuhi, kama ni wewe basi nafikiri umeshaupata. Jumamosi njema.
Mkuu SSAMBALI Nimekutumia email, lakini sijapokea majibu kutoka kwako.
 
Mkuu Godfrey,

Tuwasiliane basi maana naona kimya.

Jamaa wamesema kwa kuanzia inaweza kuwa hata 10kg. Kuna uwezekano wa kuwekeana mkataba kwa kusply tuseme kwa mwaka mmoja hadi mwili. Hivyo mwenye nguvu yake achangamkie huu ulaji.

samahani kwa ukimya. ngoja niwasiliane na jamaa kama watasema wanaweza kusupply nitakuunganisha nao moja kwa moja.
 

Nashukuru Mkuu Ssambali, bado sijapata lakini nime-forward email yangu.
 
Sawa Mkuu nakusubiria.

Kwa sasa inaonekana kuwa Dhahabu itaweza kununulika kirahisi kwa sababu ina soko tayari na mnunuzi ni mtu binafsi ila Mawese kidogo yatachelewa kwa sababu jamaa inabidi wajipange tayari kuupokea mzigo mara ukifika hapa Poland.

Ngoja tusubiri tuone nini kitatokea.
samahani kwa ukimya. ngoja niwasiliane na jamaa kama watasema wanaweza kusupply nitakuunganisha nao moja kwa moja.
 

hebu pia uzi huu https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/295636-wako-wapi-wanunuzi-wa-madini.html

mnaweza elewana.

aidha nimewasiliana na jamaa. wape wiki mbili. mambo yakiiva nitaanza wasiliana nawe kwa pm
 

dhahabu ipo,ila tujue bei kwa kila kg,gm,au tola.
 

steve mzigo wa dhahabu upo mwingi sana na unauzwa na kampuni,sema wanachukuliaje mzgo,kwa kg,gm,au tola.namansha bei yao
 
Mkuu kdany,

Nashukuru kwa majibu.

Jamaa nimeandika mapema kabisa kuwa wanataka mtu wa ku-Suply 100 kg kwa mwezi yaani kilo 100 ya dhahabu.

Bei ni muuzaji anasema na wao ndiyo wanaaza KUSHUSHA au kuanza kununua.

Mkishakubaliana nao (siyo mimi mnunuaji) basi mnawekeana mkataba na biashara inaanza.

Kuna uwezekano wa kuwa na deal hata ya mwaka mmoja hadi miwili.

Haya mambo ya Tora sijui grams hapa hayapo. Hapa bei watataka kujua kwa Kilo moja ya dhahabu ni kiasi gani.
steve mzigo wa dhahabu upo mwingi sana na unauzwa na kampuni,sema wanachukuliaje mzgo,kwa kg,gm,au tola.namansha bei yao
 

ok steve,mzigo upo na kampuni inauwezo wa kutoa hzo klo mia,na dhahabu ina asilimia kwanzia 94 had 99,bei kwa kilo ni TSH.94000000
 
Mkuu Mamilu,

Nashukuru sana kwa email. Hawa jamaa mimi mwenyewe natoa contact na ninakaa pembeni na sintataka kabisa kushiriki kwenye biashara hii. Kama ungelijua watu wenye hela ya kununua kilo 100 kwa mwezi na unafikiri utawaibia kirahisi basi utalia.

Ni mijitu iliyokuwa ikifanya kazi kwenye sehemu kama KGB ya Poland (SS) na hivyo kukutafuta na kukupata na mwisho waanze kuteketeza familia yako na kumalizia wewe mwenyewe si kazi sana kwao. Kama utapeli, basi wao ndiyo wameanzisha na sisi tunafanya kuiga tu.

Kukodisha muuwaji aje akusake si kazi ngumu kwao na watakupata tu popote ulipo.

Ningelishauri tu kama wewe huna uhakika kwenye hii biashara, basi kaa pembeni kama mie hapa. Hata kama una ukaribu na mkubwa gani Tanzania, haitakusaidia kwenye hii Mijasusi (Mafia type) ya Kimataifa.
Hi Steve kuweni makini wauzaji wengi wa dhahabu ni wapigaji
 
Wana JF,
Kwanza niwashukuru wote waliojibu huu ujumbe au kuupitia kusoma bila kuchangia.

Huyu jamaa Machinga (jamaa wa Msumbiji) kwa sasa ameondoka hapa Poland na hivyo inakuwa kama mpango mzima umekufa kwa maoni yangu na sijui alifikia wapi na contact nilizompa - Mie sikuhusika kabisa.

Kuna jamaa wawili waliweza kuwasiliana naye kuhusu ununuzi wa Dhahabu ila ikatokea kama sikosei tatizo moja kuwa inavyoonekana wanunuzi ni National Bank of Poland (Narodowy Bank Polski - NBP) au The Mint of Poland (Mennica Polska).

Hawa jamaa walikuwa wawe ndiyo wanunuzi wa dhahabu hiyo (mmoja wao) na ndiyo maana walitaka mtu anayeweza kuwaletea hadi kilo100 kwa mwezi. Ila sasa walitaka kwa bei ya chini 10% ya mnada wa UK. Ikiwa na maana hiyo asilimia 10 ndiyo wanagawana hao watu wa kati wote. Kule juu lazima tu waonyeshe kuwa wamenunua kwa bei ya Sokoni ya dhahabu na bila kujali wameinunulia wapi.

Tatizo lililozuka ni kwamba wao hawawezi kwenda Tanzania kununua ila muuzaji anawaletea, na wao wanaisafisha kwanza hadi inakuwa asilimia almost 100 safi na ndipo sasa wanapima hicho kiwango safi na hapo ndipo wanakutumia pesa wewe muuzaji. Hili lilizusha kutokuaminiana kwa pande zote mbele. Wauzaji wakiogopa kuzikwa na wanunuaji wakiogopa kuingizwa mitini huku wakiwa wameshalipa hela za Serikali.

Nafikiri hii ni biashara nzuri kwa kufanywa na kitu kama BoT maana ni Serikali kwa Serikali. Ila kwa mtu binafsi, labda uwe unamfahamu Waziri wa fedha wa Poland au Governor wake au mtu wa juu ambaye atahakikisha kuwa wakishaisafisha basi wataandika kweli kiasi haswa cha dhahabu safi iliyopatikana na kukulipa. Ilikuwa ni biashara nzuri kwani ikienda vizuri basi unakuwa na uhakika wa pesa yako bila kuzungushwa.

Nafikiri hii itakuwa imetoa ufafanuzi kwa wale watakaokuwa wanataka kunipigia simu au kuniandikia. Kama atatokea mtu BINAFSI anahitaji kitu Tanzania basi ntawajulisheni na kuwapa contact na mie nakaa pembeni. Ukifanikiwa ni heri yako na familia yako, na ukikwama basi pole maana ndiyo biashara zilivyo.
 
Ninaweza kujaribu kuulizia ila kwa kweli biashara ya madini nimetokea kuiogopa sana.

Huko wanakaa watu wa miraba minne. Ubavu huo mie sina. Nabaki kuwa kunguru mwoga na kukimbiza bawa langu.

Kuna email, simu na PM zote waweza kunipata kiurahisi.
mkuu nina interest na hii biashara ngoja nifanye utafiti kama tunaweza kufanya hii biashara
 
Hapa Kigoma mbona mawese tele tatizo ninaloliona ni suala la Kampuni,nadhani suala lahitaji mtu mwenye pesa aje akusanye halafu ndiyo awauzie. Leka tutigite!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…