Mtwara kumebarikiwa kwa kweli hakika MUNGU ni mwema.
Mfumuko mkubwa wa madini ya dhahabu umegunduliwa katika kijiji cha LUKWIKA wilayani NANYUMBU MKOANI MTWARA.
Taarifa hiyo imetolewa na kamishina wa madini mkoani mtwara ndg. Aloyce Tesha mbele ya waandishi wa habari.
Hazina hyo kubwa ya dhahabu iligunduliwa wiki mbili zilizopita na tayari wachimbaji na pamoja na watoa huduma wako eneo hilo.
Haya sasa upele umeota tena na sisi ndiyo wale tusio na kucha tuwaite tena Barick wakafanye mahandaki. Tusifanye makosa tena tupate faida sio hasara tena.
Bofya hapa: Dhahabu yafoka Nanyumbu
Hivi kwa rasilimali hizi ni kwa nini tumeamua kuwa taifa gonjwa na
dhaifu
Hivi kwa rasilimali hizi ni kwa nini tumeamua kuwa taifa gonjwa na
dhaifu
Hiyo inaitwa "Gold Rush". Usukumani huitwa rush. Mara nyingi huwa ni alluvial Gold, ni 98%. Ni vipande vya dhahabu halisi tofauti na dhahabu ya kuponda mawe yawe mchanga au vumbi na kisha kuchanganya na maji kuiyeyusha ili mwisho iwekewe mercury ili kuikusanya kama vijitonge vya ugali. Dhahabu hiyo huwa na asilimia chache. Rush huwa haidumu muda mrefu kwani uvamizi wa watu huzidi hata idadi ya elfu 50 wakati mwingine ndani ya masaa 35.
Changamoto ni sheria ya madini. Mtu (Mtanzania) haruhusiwi kushika au kuokata au kukutwa na madini kama hana leseni. Brokers, Dealers, Prospecting au Mining. Hata ukiwa unachimba choo chako na ukakuta madini ukiokota ni kosa. Ndo maana wote wanaokimbilia rush huitwa "illegal Miners". Ni lazima watafukuzwa chapo sababu za usalama ni za kweli na zitatumika kwani huchimba hovyo na hawapo organised.
Hallo Kibabhukhu unaweza nijuza taratibu na gharama za kumiliki hizi documents kwenye swala zima la madini in case already I have a company
;
1.Brokers License
2.Dealers
3.Prospecting and
4.Mining License
Ili nami nifaidi hii fursa.
Asante nawasilisha.
Kesho to utaona wawekezaji wanaanza kuwafukuza wazawa na waliogundua.