Dhahabu yafoka Nanyumbu Mtwara

Dhahabu yafoka Nanyumbu Mtwara

Wadau wa huko msingesema mapema hivi.
Sasa mambo yote yameshaharibika.
Kesho tu hapo mtaona FFU wamejazana na kuwaamuru muondoke hapo maana ninyi ni 'wavamizi' !!
Wataokaidi 'amri halali' ya polisi watazikwa wakiwa hai !!
Baadaye kidogo, wawekezaji (Barick) watatia timu (maana mwenyekiti wa bodi ya Barick ni Mr. Ole Naiko) !
Poleni sana kwa ugunduzi mhuo wa dahabu !!
 
Hii itakuwa ni balaa kwa wananchi wa huko.
 
kwanini Mtwara isijitenge na kuwa nchi kamili kama Unguja na Pemba baada ya kugundua mafuta???:biggrin:

Haina haja ya kujitenga... mafao yanayopatikana kutokana na dhahabu ya kwengine Mtwara bila shaka imenufaika nayo... tofauti na unguja na pemba... ambayo imestukizwa tu kubambikiwa hili jambo la mafuta kuwa ni la muungano...
 
Tuwaache wanakijiji wachimbe kwa masururu na machepeo baasi.
 
Waulizeni mererani wazawa wanavyojilalalia na bangi na kujifia na njaa nakujiozea meno tu wamekuwa na maisha duni kuliko kote tz hata barabara ya kwenda huko hamna na ni dunia nzima hamna panapopatikana tanzanite zaidi ya mererani nashauri kabla mwekezaji hajaanza kuchimba sera dhabiti ni kuendeleza eneo husika kwanza ensure barabara safi maji na umeme hataki ajiondokeeeee
 
Mkuu, Ninakushauri wasiliana na afisa madini yeyote ili uanze kazi mara moja. Kwa ushauri zaidi tuwasiliane. Kila kanda ina afisa madini.
 
Back
Top Bottom