Dhahabu yaibuka.

Dhahabu yaibuka.

Tatizo na sisi wananchi kiherehere sana!

Kwani mkigundua dhahabu halafu mkapiga kimya mkawa mnaokota mawe na kuweka ndani kwenu kuna ubaya gani jamani? Sasa shida inakuja ukishaiona tu mbio kwenda kutangazia umati hata kabla hujaokota mawe ya kutosha! Nyamb..ff!! Huku kwetu kuna ukoo ambao ulistukia deal la Almasi miaka ile Wazee wetu wanachezea almasi kama kete za bao, jamaa wakaokota mawe ya kutosha hasa walipomwona Williamson anaagiza wazee wampelekee na yeye anawapa mawe kwa ajili ya kuchezea bao almasi anakusanya na kuweka ndani kwake. Jamaa wakajua kumbe hii ni biashara, nao wakaanza kukusanya kwa fujo. Sasa hivi huo ukoo huwezi waambia kitu kwenye maswala ya fedha, maana inasemekana walijaza makabati na huwa wanamega kidogo kidogo na kupeleka kuuza Kenya pindi uchumi wao unapoyumba!!

Watu wa Bariadi hii watashuhudia na ukoo huo wanaujua vizuri sana!! (Hauishiwi fedha). Jamaa huwa yanazuga kama mwaka mmoja mnafikiri aaah sasa hawa jamaa zenu kwishney, mwaka ujao yanaibuka mpaka mnachanganyikiwa!!

Sasa ninyi watu wa Geita badala ya kupiga kimya mkajiokotea mawe tayari mmepiga kelele, acha mfukuzwe tumbafu nyie!!!

Stori za kijiweni bana! wahahahahahaahhhahha!
 
ccm wakisikia watasema hilo eneo ni hifadhi ya taifa hivyo ni marufuku kwa mtu yeyote kuonekana hapo na polisi watanza kulinda kwa nguvu sana hari sana na kasi sana.

Hata hivyo ni eneo la muwekezaji. Kuanzia jana kulikua na FFU wa kutosha na mabomu ya machozi yalitumika kutawanya watu.
 
Nyingine imeibuka eneo la Mwime pembeni kidogo na mji wa Kahama,jirani na Buzwagi,sasa hivi kuna zaidi ya watu elfu tano lakini nasikia dahabu ni nyingi mno.
 
Back
Top Bottom