Amoeba
JF-Expert Member
- Aug 20, 2009
- 3,288
- 791
Tatizo na sisi wananchi kiherehere sana!
Kwani mkigundua dhahabu halafu mkapiga kimya mkawa mnaokota mawe na kuweka ndani kwenu kuna ubaya gani jamani? Sasa shida inakuja ukishaiona tu mbio kwenda kutangazia umati hata kabla hujaokota mawe ya kutosha! Nyamb..ff!! Huku kwetu kuna ukoo ambao ulistukia deal la Almasi miaka ile Wazee wetu wanachezea almasi kama kete za bao, jamaa wakaokota mawe ya kutosha hasa walipomwona Williamson anaagiza wazee wampelekee na yeye anawapa mawe kwa ajili ya kuchezea bao almasi anakusanya na kuweka ndani kwake. Jamaa wakajua kumbe hii ni biashara, nao wakaanza kukusanya kwa fujo. Sasa hivi huo ukoo huwezi waambia kitu kwenye maswala ya fedha, maana inasemekana walijaza makabati na huwa wanamega kidogo kidogo na kupeleka kuuza Kenya pindi uchumi wao unapoyumba!!
Watu wa Bariadi hii watashuhudia na ukoo huo wanaujua vizuri sana!! (Hauishiwi fedha). Jamaa huwa yanazuga kama mwaka mmoja mnafikiri aaah sasa hawa jamaa zenu kwishney, mwaka ujao yanaibuka mpaka mnachanganyikiwa!!
Sasa ninyi watu wa Geita badala ya kupiga kimya mkajiokotea mawe tayari mmepiga kelele, acha mfukuzwe tumbafu nyie!!!
Stori za kijiweni bana! wahahahahahaahhhahha!