MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,580
Mapenzi haya ya sasa, si kama yale ya kale
Tumeuvika usasa, tukakosoa wa kale
Kila mtu mambosasa, hakuna katoto kale
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachua
Si wakubwa si wadogo, hata ngazi mbalimbali
Si kanisa si vigogo, wote wameenda mbali
Dunia mekuwa ndogo, waletwa hata wa mbali

Ilianzia mafuta, super kutiwa ya taa
wengi tukafurukuta, hali hiyo kukataa
Tukaujenga ukuta, biashara kukataa
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachuwa
Kama vile ikutosha, makombora yakahama
Kuanzia kwa Mugisha, mpaka kwa Bi Halima
Miili wachangamsha, bila kujali kiyama

Mume atoka na yule, penzile alichakachua
mke anagawa kule, peremende chakachua
Huyu mke wa yule, jirani achakachua
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachua.
Nilidhania ni mafuta, pekee huchakachuliwa.........