Dhahama ya kuchakachua..

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined
Jul 24, 2008
Posts
10,470
Reaction score
6,580
Mapenzi haya ya sasa, si kama yale ya kale
Tumeuvika usasa, tukakosoa wa kale
Kila mtu mambosasa, hakuna katoto kale
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachua

Si wakubwa si wadogo, hata ngazi mbalimbali
Si kanisa si vigogo, wote wameenda mbali
Dunia mekuwa ndogo, waletwa hata wa mbali
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachua

Ilianzia mafuta, super kutiwa ya taa
wengi tukafurukuta, hali hiyo kukataa
Tukaujenga ukuta, biashara kukataa
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachuwa

Kama vile ikutosha, makombora yakahama
Kuanzia kwa Mugisha, mpaka kwa Bi Halima
Miili wachangamsha, bila kujali kiyama
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachua

Mume atoka na yule, penzile alichakachua
mke anagawa kule, peremende chakachua
Huyu mke wa yule, jirani achakachua
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachua.

Nilidhania ni mafuta, pekee huchakachuliwa.........
 
kamanda wa mashairi, chakachua ni imani
hata ukikuta chagga, angalia na kitanda
cheki hata kanda, za video na kaseti
chunguza maziwa, hat nazi za kisasa
chakachua ni imani, kama ile ya bohora
 
kamanda wa mashairi, chakachua ni imani
hata ukikuta chagga, angalia na kitanda
cheki hata kanda, za video na kaseti
chunguza maziwa, hat nazi za kisasa
chakachua ni imani, kama ile ya bohora

Nakiri kuwa ni kweli, chakachua ni imani
Na pia kuna ukweli, huwa ukweli imani
Hata ukenda kwa reli, itabakia imani
imani hulizaa tendo, mapenzi kuchakachua kamanda.

So ikipatikana dawa ya kuzuia uchakachuliwaji wa mafuta, tutaidai na ile ya kuzuia kuchakachuliwa kwa mapenzi ikiwemo kukimaliza chama maarufu cha Infidelity na kile cha nyumba ndogo bila kusahau kile cha wapenzi wachanga.
 
Mapenzi ya chakachua, sababuye wanawake,
Kujifanya wanajua, wachanganya na makeke,
Kisha waangukia pua, kila kitu mwakemwake,
Mapenzi ya chakachua, Hapa ni nyumbani kwake.
 

kamanda wenda mrama, hii sasa nakujuza
tena chepuka mapema, kwani wewe si ajuza
pitia sheria mama, kile chama chapendeza
chakachua sio infi, na infi si chakachua

chunguza sana kwa ndani, halafu pima imani
infi hurejesha amani, na pia huleta imani
infi ni jenuini, chakachua ina "lakini"
chakachua sio infi, na infi si chakachua

wa infi hutoa yote, chakachua haiwezi
chakachua ni kugeza, bali infi ni kuweza
hebu jaribu chakachua, halafu jaribu pia infi
chakachua sio infi, na infi si chakachua
 

Infii na chakachua, sawa mafuta na maji,
Infi ni kitu murua, chakachua dogo mtaji,
Infii ni mila sawia, chakachua siyo kipaji,
Kamanda Acid Hongera, Chama kitakutunuku.
 
Mume atoka na yule, penzile alichakachua
mke anagawa kule, peremende chakachua
Huyu mke wa yule, jirani achakachua
Wote tumekuwa hodari, mapenzi kuchakachua.

Nilidhania ni mafuta, pekee huchakachuliwa.........

Penzi la kuchakachua, ndilo lenye utamu,
Hutuchakachui kila siku, bali ni kwa hamu,
Mie nina uzoefu, wana JF mfahamu
Chakachua ni tamu, hasa akiwa binamu

Hii haijaanza leo, bali tangu enzi za adamu,
Isipokuwa mambo yalifichwa, watoto wasifahamu,
Leo hii mambo hadharani, watu hawaogopi jehanamu
Chakachua ni tamu, hasa akiwa binamu
 
MJ1... usiogope infii, ogopa chakachua, maana chakachua sio halisi lakini infi ni genuine!!! unaweza kuchakachuliwa hata kwenye ndani ya ndoa lakini kwenye infi mazee watu na kitu vyote ni genuine
 
MJ1... usiogope infii, ogopa chakachua, maana chakachua sio halisi lakini infi ni genuine!!! unaweza kuchakachuliwa hata kwenye ndani ya ndoa lakini kwenye infi mazee watu na kitu vyote ni genuine

Unajua MJ1 anataka kulinganisha uchakachuaji na infii....havilingani wala havichangamani kabisa. Ni sawa na mafuta na maji!!:welcome:
 
Hongera MJ1 naona na wewe ni malenga mzuri sana Keep it up swirry
 
hicho kipengele cha mwisho MJ1 nimekipenda sana...
 
Mh huku nahisi kama nimepotea njia! :confused2::confused2:
Am sure MJ1 nimemuelewa vizuri lakini the rest mnanichanganya>>>:A S-confused1::A S-confused1::sleepy::sleepy:
 
binaadamu wanjanja, wazuri wa kuigiza
kitu kimoja kianza, vyengine vitamaliza,
mafuta yalivyofanzwa, mapenzi yaendeleza
mapenzi kuchakachua, ni ujuzi wa kuwaza.

sheria za ubunifu, chanzoni hazijatanzwa
iwe kwa muuza beef, au muokota chenza
utapita usanifu, mawazo kuendeleza
mapenzi kuchakachua, ni ujuzi wa kuwaza
 
Mh huku nahisi kama nimepotea njia! :confused2::confused2:
Am sure MJ1 nimemuelewa vizuri lakini the rest mnanichanganya>>>:A S-confused1::A S-confused1::sleepy::sleepy:

:becky::becky::becky: pole sana basi na wewe akili yako inabidi ichakachuliwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…