Dhahama ya kuchakachua..


kwanini si chakachue, naye fikiri aweza?
ubunifu kwake yeye, upo umejituliza
mwanamme si pekee, faida anae waza
kama ni kuchakachua, wote wana nguvu sawa.

mwanamke siku hizi, ni mjasiriamali
hesabu haimkwazi, sio kama wa awali
chakachua ya mapenzi, mtaji wafika mbali
kama ni kuchakachua, wote wana nguvu sawa.
 
MJ1 hongera kwa mashairi mazuri and very realistic!nilijua kuwa Kaizer na Gaijin nao ni wazuri ktk hilo lkn nimeshangazwa na Acid na Asprin kumbe walikuwa hawavumi lkn wamo!!!!!!!!!!!BIG UP
 
Hahahahaa naona nimekushika pabaya Kamanda...... nipe tofauti ya chakachua na infii tafadhali loh

aah kamanda, mbona somo liko wazi?? kuchakachua ni kuongeza kitu chenye ubora wa chini kwenye prime... mfano mzuri kama vile kutumia zana zisizo (madude feki, pingu, nk. kwenye love marking. infii ni ile dhana na tendo la kushare nje ya mstari ukiwa na lengo zuri sana la kuboresha nyumbani, either kupunguza visirani, au kuongeza ujuzi

OOppps you missed me again... and probably infii regulations hujazielewa... Infii by no means replaces the prime love and therefore you can never compare the two. in actual facts infii ni kama chachandu kwenye pilau au maziwa kwenye kahawa... lengo lake kuu ni kuboresha na sio kushibisha

Kamanda hapa napinga, kwa infii kutoa yote
kutoa yote ni kazi, yahusisha moyo wote
Kama hunayo hisia, huwezi toa yote kamanda.

unaona sasa kamanda?? kila sehemu lazma utoe yote, tofauti na chakachua kwani haina ubora.. infii na prime kote lazma utoe vyema

Kumbuka huwezi kutema bigG yako kwa karanga za kuonja
 
Deodat karibu, ukaribie na kiti
unijuze kwa karibu, ngoja nibebe na kiti
Mzoefu na tabibu, utujuze kitikiti
Chakachua ya binamu, vipi ikawe ni tamu?

chakachua ya binamu, vipi nayo iwe tamu?
kamanda kweli mumu, sasa nhsafahamu
sikuwazia humuhumu, kwamba si wote wagumu
binamu nyama ya hamu, kamanda chukua hiyo
 

Mwanamke asilia, kaumbiwa wa nyumbani,
kuitunza familia, na kutoa burudani,
mume kumtimizia, yajiriyo nje ndani,
Mwanamke chakachua, si mwanamke bora.

Wanyama wa makondeni, mfano wanatolea,
majikeye asilani, hayafanyi chakachua,
na madume makundini, majike yanachangia,
Mwanamke chakachua, si mwanamke bora
 
Seriously .... I rest my case. Totally defeated I admit.

Watu mtadhani mmeiendea course!!
 

Your avatar na hili shairi vimekompliment each other balaa

ngoja nikachakachue nirudi... ANGALIZO, CHAKACHUA SIO INFII
 
mie nimebaki nimeduwaa, ni huyu huyu kichpin?....MJ1 na Gaijin mnanikosha sana, Acid nae wamo khaa balaa kubwa hili, akija Fidel hapa atamwaga utumbo wake mpaka bac.
 

asili ya binaadamu, chimpanzi wajua.
yeye bila kulaumu, mabwana achakachua
kuikidhi yake hamu, apendacho ajilia
penzi la kuchakachua, na litumike kwa wote

sauti ya mngurumo, au mnene mkia
mwingi wake mtazamo, akionapo kifua
mawazo yashinda humo, vipi atakilalia
penzi la kuchakachua, na litumike kwa wote

dhana hii ya usawa, sasa sio ngeni tena
mwanamke ana power, kuishi anavyopenda
baolojia kapewa, ya dume yote kutenda
penzi la kuchakachua, na litumike kwa wote

:tonguez:
 
mie nimebaki nimeduwaa, ni huyu huyu kichpin?....MJ1 na Gaijin mnanikosha sana, Acid nae wamo khaa balaa kubwa hili, akija Fidel hapa atamwaga utumbo wake mpaka bac.

leo nakula nao sahani moja hawa wachakachuaji mashuhuri ................lol

Nakuwakilisha Nyamayao manake naona mduao wako mkubwa!
 
leo nakula nao sahani moja hawa wachakachuaji mashuhuri ................lol

Nakuwakilisha Nyamayao manake naona mduao wako mkubwa!

wacha tu....niwakilishe dearest coz cna moja wala mbili kwenye haya mambo, natoa tu macho hapo....wakimbizeee mama.
 
Eti huwezitema BigG yako kwa karanga za kuonja.... Acid yaani huu ni ujumbe wa wiki kwa kweli.

naomba hati ya kuuweka kwenye signature yangu pleas...... nitakuacknowledge
 

Kaditama wahisani, naomba kuwakimbia,
vilivyomo mafrizani, tayari vimeshapoa,
vinapendeza kooni, kwa kasi vikiingia,
Infii asilani, si sawa na chakachua.

Vikishapanda kichwani, lojistiki zaanzia,
kina eliza yakini, mipango najifanyia,
napeleka mjengoni, nao najichakachua,
nikirudi nyumbani, mwepesi najifikia!

Mama matesha tulia, mumeo niko milani,
infii najifanyia, ila sitakurubuni,
nikisha kujisevia, naingia utunduni,
kitanda tukiingia, nakupa maburudani.
 
Naombeni kuuliza jamani , hivi kuchakachua maana yake hasa ni nini?
 
aaahh swahiba... wanasema riski fil' manyaat aisee

ndo naingia home baada ya kazi ngumu sana ya kuangalia europa league

Teamo is seriusly considering the offer to become a visiting professor wa infii at the university of Washington, GA
 
Asprin is on FIYAH! ......
Hahahaha!Asprin is HOT! You are :welcome:
aaahh swahiba... wanasema riski fil' manyaat aisee

ndo naingia home baada ya kazi ngumu sana ya kuangalia europa league

Teamo is seriusly considering the offer to become a visiting professor wa infii at the university of Washington, GA

Kamanda naona somo lilieleweka..... Chakachua si sawa na Infii......Thats 2010 Acid's motto!:hand:
 
Hahahaha!Asprin is HOT! You are :welcome:


Kamanda naona somo lilieleweka..... Chakachua si sawa na Infii......Thats 2010 Acid's motto!:hand:
swadaktaaaa

bado namsubiri kaizer aje na ledger ya chama na waliolipia ndio nichape lapa kuelekea chamber
 
Kaizer arent you back yet??

by the way Avatar yako inanikwaza yaani kila nikiiona nasikia kiu!!


Sikujua chakachua, hadi jamvini majuzi!

Ndipo sasa nikajua, kumbe kwataka ujuzi!

Sasa wananitibua, kulandisha na mapenzi!

Mafuta kuchakachua, sio lazima mapenzi!


Ndio ninasema tena, Sio lazima mapenzi
Wapi wetoa hi' dhana, unijuze mi mkwezi?
Ili tutapokutana, wote tuimbe utenzi,
Twimbe tenzi za mapenzi, sio kuchakachuana!

MJ1 nakuasa, usikubali kuchakachuliwa!
Tena nakupiga msasa, usije sema hukuambiwa
Mafuta yachakachuliwa sasa, lakini sio vitumbuwa,
Chukua chako kikapu, 'kitaka nitakutuwa!

Usidangaywe na rangi, tamu ya chai sukari,
Wahaya hata Warangi, ni moja yao futari
Basi njoo Mkamangi, nikupigie zumari!:violin:
Chukua chako kikapu, 'kitaka nitakutuwa!
 


The Following 4 Users Say Thank You to Gaijin For This Useful Post:

Acid (Yesterday), Asprin (Yesterday), Kaizer (Today), MwanajamiiOne (Yesterday)​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…