Dhahama ya Ndoa...

Dhahama ya Ndoa...

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Posts
4,873
Reaction score
1,217
Jana limezuka tafrani mtaani kwetu Jamaa (Mr stephano) akimtuhumu mke wake si mwaminifu katika ndoa.Akieleza kinaga ubaga kilichompelekea kuzua taflani hilo ni kwamba Mke tangu amemuoa ni MIAKA 10 Wamejaaliwa kuzaa watoto 3 mmoja wa kike wawili wa kiume lakini cha kushangaza hao watoto wote wanafanana Rafiki zake wa karibu.Hakuna hata mmoja aliefanana nae ina mana yeye analea watoto wa vidume wenzake.
Dhamama ya ndoa

Je ungekuwa wewe ungeamua nini?
 
Asikasirike ni kawaida mbona waha wanaposafiri kwa treni kwenda Kigoma kile kitendo cha kukaa kwenye behewa kwa siku tatu na kwa muda mrefu kinawafanya wote wafanane sura
 
Mwanamke mjamzito akimchukia mtu anazaa mtoto aliefanana nae. Asiwe na wasiwasi.

Ila jamaa atakuwa mmang'ati eeh? Manake huku kwetu wanafananisha hadi nywele!
 
Ningeamua watoto wote warejeshwe kwa baba zao haraka iwezekanavyo-kisha watafutwe wengine halali!
 
Atumie busara aende hospitali na kupima DNA hiyo imsaidia kugundua kama alisaidiwa na marafiki zake
 
Asilalamike sana huenda bastola yake haina risasi so wife kaamua kumuondolea aibu....natania tu jamani
 
Hivi bongo kuna vipimo vya DNA? Na kama vipo, nini hatua za kuchukua kupata vipimo? Hospitali gani?
 
Jana limezuka
tafrani mtaani kwetu Jamaa (Mr stephano) akimtuhumu mke wake si
mwaminifu katika ndoa.Akieleza kinaga ubaga kilichompelekea kuzua
taflani hilo ni kwamba Mke tangu amemuoa ni MIAKA 10 Wamejaaliwa kuzaa
watoto 3 mmoja wa kike wawili wa kiume lakini cha kushangaza hao watoto
wote wanafanana Rafiki zake wa karibu.Hakuna hata mmoja aliefanana nae
ina mana yeye analea watoto wa vidume wenzake.
Dhamama ya ndoa

Je ungekuwa wewe ungeamua nini?

Aache roho mbaya,anaona shida kuwasaidia rafiki zake wakaribu kulea?
 
Wivu unamsumbua.

Ni kweli maana kama unamhisi mtu vibaya kila unapomwangalia mtoto unaona anafanana na rafiki yako kwa kuwa wakati unamwangalia unavuta hisia ya rafiki yako. Hii ni sawa na ndoto unaota vitu ambavyo umekuwa ukiviona au kusimuliwa kwani mtoto wa kijijini hawezi ota amegongwa na gari kama hajawahi kuona gari sana sana ataota amegongwa na nyoka
 
Labda imetokea tu automaticaly inawezekana sura nazo zinaambukiza siku hizi!
 
Back
Top Bottom