Dhambi ya Ufisadi yaanza kutafuna Habari corporation

....bagenda alikuwa awe juu..wiki ijayo alikuwa aje na hilo gazeti..soon after redio na kituo cha televisheni ,bahati mbaya kituo chote na news room vimeungulia humo..kama kweli mnavyosema kuwa naye nii malaya basi safari atakuwa alikuwa amepata bwana mwenye pesa .....si vibaya tukamjua ni nani anayeweza "kuoa" hadi wanaume wenzake!!!!

loo tutaona mengi!!!
 

GIDEON SHOO anatarajiwa kurudishwa HABARI CORP kuwa DIRECTOR!
 

kinachosikika ni kwamba baadhi ya waandishi wa vyombo vya habari wamehongwa jumla ya ml30 na BWANA MAMVI...na inasemekana HABARI CORP wapo waandishi watano waliokula pesa za MAMVI....TAGALILLE amejiuzuru baada ya kuambiwa akawe mhariri wa THE AFRICAN hivyo kuona kuwa kama wamemshusha cheo na kuwa chini ya BALILE,lakini hiyo ilikuwa ni kumtafutia sababu ya kuondoka HABARI CORP,ilikuwa inaeleweka kuwa TAGALILLE hasingekubali kuwa chini ya BALILE
 
Navyofahamu,Bagenda alirubuniwa kutoka kundi la waandishi wenye uchungu na nchi na kuingia kwenye Mtandao.Kwa jinsi Mtandao ulivyoparaganyika,ni vigumu kujua "kaolewa" na nani,lakini ni rahisi kuhisi kwamba "bwana yake" atakuwa mtu wa Mtandao pia.Kulikuwa na tetesi za Mamvi kuanzisha chombo cha habari ambacho kingefanya kazi na Habari Corporation kwa namna IPPMEDIA inavyofanya kazi na MEDIA SOLUTIONS (Kulikoni na ThisDay)..

Ni rahisi ku-speculate kwamba Mamvi anataka kugombea urais 2010 kwa njia yoyote ile,ndani au nje ya CCM.Ama kweli ushirika wa wachawi haudumu maana laiti mtu angefikiri haya 2005 angeonekana anaota ndoto za mchana.
 


yap hizi mbinu muungwana na mvi wanajua vema kuzitumia....sasa kwa kuwa wapo kwenye timu tofauti..kaaz kweli..waandishi vishoka waandae matumbo tu!!!!...na wale wanaopenda kuwa included kwenye safari za kitalii ulaya nafasi ndio hiii...wamuone salva kwa niaba ya....wanavuna kote kote !!!! duh ..safari ndefuu!!
 


....latest za wiki hii ni kuwa NAZIR KARAMAGI alikuwa kwenye hatua za mwisho kufungua media house ya nguvu....wakuu inawezekana ikawa ndio hii ya bagenda nini??....na kama ndivyo kutakuwa na uwezekano mkubwa kuwa hii ingekuwa linked na mtandao maslahi ambao sasa wanapigana kurudi....

sasa wakuu kama hiyo media house ingekuwa against serikali na ukijua wangekuwa na radio na tv...huu moto niaje..click!!!!
 

ATILIO TAGALILE ndo alikuwa Mhariri Mtendaji wa Habari Cooperation, tunaweza kusema kwamba yeye ndo alikuwa CEO wa habari coops. Kwa namna yoyote ile, asingeweza kukubali kuwa mhariri wa The African maana hiyo ni "demotion".Pamoja na hayo, ATILIO ni mwandishi na mtangazaji ambaye ameshafanya kazi kwenye vyombo vikubwa vya habari kama Sauti ya ujerumani, kwa hiyo naamini hana njaa kama za akina BALILE.Anaweza kurudi serikalini Daily News maana alishawahi kuwa mhariri9Feature Editor) wa Daily News.
 
Mnyoofu, wataje tu tuwape hongera zao please...kama wamefanya jambo la pongezi, why unaficha majina? Unawanyima haki yao ati!

hapa ndipo ambapo huwa naikubali JF. We dare to talk openly,lete majina yao jamvini tuwape pongezi zao. Maana jambo hili ni muhimu sana na linahitaji kupongezwa.Unapoona ujasiri wa kifisadi unatoweka miongoni mwa waandishi wa habari basi ni hatua kubwa sana.
 
Madilu mkuu wangu,kula tano.
Kwa kweli nimekupenda sana kwa hiyo gharama yako ya kukununua.SUBUTU NANI ATASOGEA KWENYE HIYO OFA ULIYOTOA! wewe ni mzalendo kweli.
 

Huyu ndiye Bagenda: http://www.chadema.net/makala/kafulila/david_4.html kama kuna makala nyingine iliwahi kuandikwa ikimueleza Bagenda ni nani- nadhani tungeipata ile ingetupa picha kamili juu ya mtu huyu. Ni kweli kile chombo cha habari kilichounga pale ushirika ni cha Karamagi kwa kumtumia Bagenda

Asha
 

Balile sounds like Balali and they are both CORRUPT Shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiit!!!!
 

Eh? Jamani kazi imenizidia labda nimepitwa... katika ile moto ya juzi katika jengo la UShirika kuna chombo cha habari kimeungua? Mhh! Hii kweli hujuma! Lakini kwa vile ni ya mafisadi wacha wanedele kuhujumiana
 
Ndiyo, hii habari ni ya kweli kabisa. Lakini kainachotia moyo ndicho hicho kwamba je wakiwa wengi watakaokuwa wamegomea huo mpang itakuwa heshima kwa taaluma ya habari aliyoitukana Lowasa kuwa imejaa udaku, halafu inashangaza sasa wanapotumia mamilioni kutafuta waandishi wawasafishe. AJABU!

lAKINI INASHANGAZA SANA KUONA HUYU KIJANA MSOMI BALILE KAPATWA NA WEHU NA UMBUMBUMBU KIASI GANI!
Hivi inakuwaje unauza utu wako kwa hizi hela chafu zinazonuka, au ndo kina Salva hawa wanaoaibisha taaluma hii, walah, mola awalaani!

Tulione hili la Habari corp kama litakuwa ushindi wa kweli kwa wanahabari, isije ikawa nguvu ya soda, tuone!
 
kusema kweli hii ni habari nzuri sana kwa wale wazalendo maana kusema kweli Habari Corp. ilishakosa muelekeo mara baada ya kutoka kwa Jenerali na wengine kadhaaa.
 
..ukishanunua waandishi,what next? kununua wananchi au?

Inategemeana na wananchi wenyewe! Kumnunua mheshimiwa Idimi ama Mlalahoi yataka moyo!



.."penye dhiki penyeza rupia"

Sawasawa, ila sio kila penye udhia unaweza kupenyeza rupia. Kuna mahali rupia huwa zinadunda!

Eh? Jamani kazi imenizidia labda nimepitwa... katika ile moto ya juzi katika jengo la UShirika kuna chombo cha habari kimeungua? Mhh! Hii kweli hujuma! Lakini kwa vile ni ya mafisadi wacha wanedele kuhujumiana

Mkuu, hata mie nashangaa! Yaani tunapitwa na mambo mengi sana. Sikuwa nafahamu kwamba kuna vyombo vya hbari vipya pale Ushirika.

Kuhusu Deodatus Balile, nakumbuka walishachambana sana na Prudence Karugendo kwenye Tanzania Daima, kuhusu kununuliwa na konunulika! Prudence aliponda sana kitendo cha Balile kujipendekeza kwa 'wakubwa', kwa sababu alikuwa anadhalilisha taaluma yake kwa kununuliwa. Walilumbana kwa wiki kadhaa, hadi ikabidi mhariri asitishe mjadala huo.
Baadaye sasa nikasoma makala ya Balile akijiengua kutoka Free Media na kusema atafanya kazi zingne. Sikuwa najua kwamba hizo 'Kazi nyingine' ni za Mvi na Muirani.
Pole yake!
 
Waliojiuzuru Habari Corporation ni Atillio Tagalile, Chrisostom Rweyemamu na Ben Mhina (Mkurugenzi wa usambazaji) baada ya kuibuka mzozo wa kutaka kampuni ishiriki kikamilifu kuwasafisha mmiliki pamoja na EL. Wapo wanaotaka yafuatwe maadili ili stori za ufisadi ziandikwe kama kawa, na wapo wanaotaka ufanyike usafishaji (nadhani ni human laundry). Inasemekana wengine wengi zaidi wanatarajiwa kujiondoa kwenye kampuni hiyo.

balile anadaiwa kuviuruga kampuni kwa kuwachongea wenzie kwa RA, na mawasiliano yake ya moja kwa moja na RA yanadaiwa kuwakwaza wengine kwa kuwa hafuati channels of communication.

Baadhi ya article zake za Monduli zimegomewa kuchapwa, na ndipo moto ulipowaka kwenye mkutano wa last week. Amejitetea kuwa alibanwa wakati akijaribu kuwatetea waandishi wa kujitegemea, na kwamba eti alibanwa kama Karamagi, na anasema hajutii yanayotokea. Atilio amemshauri Balile aachie ngazi kwa kuwa wafanyikazi wengi wanamuona yeye amechafua hewa toka aingie pale.

Hivi haya majina yana uhusiano? (daudi balali na deodatus balile...naona herufi zimehamishwa tu kiufisadi) lol...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…