Dhambi zinavyotengeneza ukuta wa kuzuia Baraka za Mungu katika maisha ya Mtu

Dhambi zinavyotengeneza ukuta wa kuzuia Baraka za Mungu katika maisha ya Mtu

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,237
Reaction score
1,744
Yer 5:25 SUV
[25] Maovu yenu yameyageuza haya, na dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate.

Ujumbe huu ulikuja kupitia kinywa cha nabii Yeremia kwa taifa la Yuda, watu hawa walikuwa wamemwacha Mungu na kufanya mambo yasiyofaa mbele zake.

Yale maisha yao au kule kupotoka kwao kiroho, kulizuia zile baraka zilizoahidiwa au zilizokusudiwa kwao, mvua ilikuwa inyeshe haikunyesha kwa wakati wake, mavuno yalikuwa adimu, amani kwao ilipotea kabisa.

Kilichofanya wasipate zile baraka za Mungu walizoahidiwa ilikuwa ni kwa sababu ya maisha yao ya dhambi, hali ya ukame ikawa imeingia kwao na kukosa amani kabisa.

Dhambi haipaswi kutazamwa kama kosa la kimaadili tu, dhambi inapaswa kufahamika kwetu kuwa inavunja kabisa uhusiano wetu wa kiroho au wa kiagano na Mungu. Unaweza kuona jinsi gani inakuweka mbali na Mungu, ule uhusiano wako mzuri unakosekana kabisa na kubaki peke yako.

Katika agano la kale tumeona baraka nyingi zilihusishwa na utii wa agano, yule ambaye angeenda kinyume ilikuwa ni dhambi iliyoondoa agano, ukiharibu agano huwezi kupokea baraka za Mungu. Nasi leo ukiharibu uhusiano wako na Yesu, usitegemee kuona baraka za Mungu katika maisha yako.

Ieleweke kwamba, dhambi ni ukuta mbaya sana kati ya mwanadamu na Mungu, mtu akifanya dhambi amejiwekea ukuta mwenyewe wa kumfanya asiweze kuhusiana tena na Mungu wake. Bila toba na kuacha mambo mabaya, ukuta huo utaendelea kuwepo siku zote.

Yer 3:12-14 SUV
[12] Enenda, ukatangaze maneno haya kuelekea upande wa kaskazini, ukaseme, Rudi, Ee Israeli mwenye kuasi, asema BWANA; sitakutazama kwa hasira; maana mimi ni mwenye rehema, asema BWANA, sitashika hasira hata milele. [13] Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi BWANA, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti yangu, asema BWANA. [14] Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema BWANA; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni.

Ukigundua umemtenda Mungu dhambi, unapaswa kuchukua hatua haraka sana, ili kuondoa mpaka au ukuta mbaya uliopo kati yako na Mungu. Hili halimhusu mtu mwingine ni wewe na Mungu wako, ukipuuza umechagua kuteseka katika maisha yako.

Kumbuka baraka zetu za kiroho na kimwili zipo katika Yesu Kristo, ukiharibu uhusiano wako na Yeye uwe na uhakika utakuwa umechagua kuharibu zile baraka chache ulizopokea na kuondoa uwepo wa Mungu katika maisha yako. Jambo ambalo ni hatari sana kwako.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
unamaliza wino tu Kama usipotoa definition what is Dhambi ? na imeshugulikiwa vipi according to bible
 
Back
Top Bottom