Uchaguzi 2020 Dhana ya kushinda Uchaguzi bila Kupingwa ni hatari kwa Usalama wetu

Mtukudzi

Senior Member
Joined
Nov 14, 2013
Posts
103
Reaction score
408
Kushinda uchaguzi bila kuchaguliwa kwa kisingizio cha kupita bila kupingwa ni jipu ambalo yafaa litumbuliwe haraka ili kuleta usawa na kushamirisha amani ya Nchi yetu.

Haiingii akilini kuwa mtu anaweza kutumia mbinu wazi au fiche kudhibiti washindani wenzake na kisha aonekane kuwa ni chaguo la wapiga kura wote

Tumesikia mtu anauawa huko Ukerewe katika kile unachoweza kusema ni harakati za kutengeneza mazingira ya "kupita bila kupingwa". Hii ni hatari kwa usalama wa nchi.

Ifike wakati hata kama hakuna mgombea aliyejitokeza au wagombea wanakosa sifa basi tufuate utaratibu wa kura za Ndiyo/Hapana ili kuwadhibiti wagombea wetu na hatimaye kudhibiti amani na hatimaye kupata viongozi waliochaguliwa.

Imani yangu ni kuwa jambo hili lina umuhimu na ndiyo maana Mwalimu Nyerere hakuwahi kupita bila kupingwa hata kama hakuwa na mtu aliyejitikeza kumpinga. Alijua kuna wapiga kura wanaompinga. Si huyo tu hata Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hata juzi Magufuli alipigiwa kura za Ndiyo/Hapana kwenye mchakato wa kuteuliwa kuongoza duru ya pili. Hata Mzee Sumaye huko Chadema alipigiwa kura za namna hiyo. Hiyo Ndiyo democracy ya kweli.

Tujitafakari sana kwa sababu kupita bila kupingwa ni bomu ambalo limeanza kuota mizizi!

Soma pia Kupita bila kupingwa - this too is democracy?
 
Huku ni kulalamikia kule tulikoangukia badala ya kule tulikojikwaa. Shinda iko kwenye Tume ya Uchaguzi. Kama Kuna mtu, kikundi au taifa linalotaka kutusaidia sisi watanzania Basi litusaidie tupate katiba na tume huru ya uchaguzi.

Mimi nikiiangalia CCM Leo naona inatumia mbinu zilezile walizozitumia makaburu kuendelea kubaki Afrika kusini na wareno walivyokuwa wameng'ang'ania kuzitawala Mozambique, Angola. CCM leo hii inafanya kila kitu kilichofanywa na wakoloni ili kuendelea kutawala.

Vyama vyooote hivi vya siasa tukivyonavyo mgombea atapitaje bila kupingwa? Kuna tofauti gani Ni makaburu? Mbinu wanazotumia zinaendelea mbaya zaidi kila wapigakura wengi wanapoendelea kuelemika kuhusu democracy. Zinaendelea kuwa za wazi kutoka kuwa za kificho.

Kwanini ni CCM tu inayopita bila kupingwa na sio vyama vingine kwenye majimbo yote?
 
Kushinda uchaguzi bila kuchaguliwa kwa kisingizio cha kupita bila kupingwa ni jipu ambalo yafaa litumbuliwe haraka ili kuleta usawa na kushamirisha amani ya Nchi yetu.

Haiingii akilini kuwa mtu anaweza kutumia mbinu wazi au fiche kudhibiti washindani wenzake na kisha aonekane kuwa ni chaguo la wapiga kura wote

Tumesikia mtu anauawa huko Ukerewe katika kile unachoweza kusema ni harakati za kutengeneza mazingira ya "kupita bila kupingwa". Hii ni hatari kwa usalama wa nchi.

Ifike wakati hata kama hakuna mgombea aliyejitokeza au wagombea wanakosa sifa basi tufuate utaratibu wa kura za Ndiyo/Hapana ili kuwadhibiti wagombea wetu na hatimaye kudhibiti amani na hatimaye kupata viongozi waliochaguliwa.

Imani yangu ni kuwa jambo hili lina umuhimu na ndiyo maana Mwalimu Nyerere hakuwahi kupita bila kupingwa hata kama hakuwa na mtu aliyejitikeza kumpinga. Alijua kuna wapiga kura wanaompinga. Si huyo tu hata Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hata juzi Magufuli alipigiwa kura za Ndiyo/Hapana kwenye mchakato wa kuteuliwa kuongoza duru ya pili. Hata Mzee Sumaye huko Chadema alipigiwa kura za namna hiyo. Hiyo Ndiyo democracy ya kweli.

Tujitafakari sana kwa sababu kupita bila kupingwa ni bomu ambalo limeanza kuota mizizi!

Soma pia Kupita bila kupingwa - this too is democracy?
Tuwakatae washenzi hawa waoga wa demokrasia ccm na vibaraka wake.
 
Back
Top Bottom