Hata kama hamtaki, au kwavile mnapenda kuingiza siasa kwenye kila jambo, hapa nitarudia tena!
Kama hoja yako ni kutokana na issue ya Samia vs Ndugai, pale HAKUNA MHIMI ULIONGILIWA...
Ndugai sio MHIMILI kama mnavyojaribu kuaminishana bali BUNGE NDIO MHIMILI.
Mbunge anapoongea au kufanya kazi ya Kibunge NDANI YA BUNGE, ndipo anakuwa amefanya au kusema kwa niaba ya Mhimili!! Na anaposema kwa niaba ya Mhimili, hapo ukimwingilia au kum-challenge ndo utakuwa unau-challenge Mhimili kwa sababu, ingawaje Mhimili ni Bunge na sio Mbunge lakini bado Bunge haliwezi kuwa Bunge bila Wabunge!!
Ni kutokana na hilo, ndo maana Ibara ya 100(2) ya Katiba yetu inasema:
Hapo utaona wazi kwamba, Comfort Zone kwa Mbunge ni Ndani ya Bunge! Akiwa ndani ya Bunge anakuwa anafanya kazi ya kibunge kwa niaba ya Bunge ambalo ndilo Mhimili!
Nje ya hapo, kama ilivyotokea kwa Ndugai, Mbunge/Spika au Ndugai mwenyewe atakuwa analindwa na Ibara ya 18(1) ambayo inazungumzia Uhuru wa Kutoa Maoni kwamba:-
Kwahiyo Samia angeweza kuhukumiwa kwa kuingilia Uhuru wa Kutoa Maoni na sio kuingilia Mhimili kwa sababu Ndugai kaongea aliyoongea akiwa na watu wa jamii yake kwenye mambo yao!
Hata hivyo, kumhukumu Samia kwamba ameingilia uhuru wa kutoa maoni inabidi utoe ushahidi kwamba Samia aliagiza Ndugai akamatwe au ajiuzulu!!
Kinyume chake, nilichokiona kwa Samia ni kile kile alichofanya Ndugai! Ndugai katumia uhuru wake wa kutoa maoni kumshangaa Samia na Samia nae akatoa uhuru wake wa maoni kumshangaa Ndugai!
Kama Ndugai ana uhuru wa kutoa maoni na kumshangaa Samia na mambo yake ya kukopa kopa, kwanini Samia nae asiwe na uhuru wa kutoa maoni na kumshangaa Ndugai kupinga hadharani jambo ambalo ameshiriki kupitisha?
Kama tunaamini Rais ameingilia Mhimili, kwanini Spika nae asionekane ameingilia mhimili mwingine?!
Hilo la kumshangaa Ndugai ndio linatufikisha kwenye kitu kinaitwa Collective Responsibility! Tuache ushabiki, Ndugai amekiuka misingi ya Collective Responsibility ya uongozi!!
Ibara ya 62(1) inasema Bunge litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge! Kwa maana nyingine, SSH nae ni sehemu ya Bunge! Na kifungu kidogo cha 3 cha ibara husika kinasema:-
Utaona hapo, jambo lolote halitahesabiwa kwamba limeamuliwa ipasavyo hadi limeamuliwa na Wabunge na vilevile Rais kwa sababu kama tulivyoona hapo juu, Rais na mwenyewe ni sehemu ya bunge.
Utaratibu ni kwamba, wakati wa Bunge la Bajeti ukifika, Waziri wa Fedha ataenda bungeni kusoma bajeti ya Makadario ya Mapato na Matumizi! Kwavile hata baada ya miaka 60 ya uhuru bado tunakuwa na budget deficit, katika soma yake ya bajeti hatimae Waziri atafikia sehemu kama hii:-
View attachment 2076879
Na akishamaliza kusoma, waziri atatoa hoja na wakati ukifika, Wabunge wataijadili hotuba ya waziri na mwisho wa yote, Spika atawauliza wabunge wanaoikubali bajeti wasema ndiyo na wanaoipinga waseme sio!
Sasa kama tujuavyo wabunge wetu, ikishafika hapo itakuwa NDIYOOOOOOOOOOOO!! Kwa maana nyingine, Taasisi inayoongozwa na Spika, yaani Bunge, ambalo ndilo Mhimili, hatimae linamkubalia Waziri wa Fedha pamoja na mambo mengine, AKAKOPE PESA NJE!!
Sasa hapo ndipo inakuja dhana ya Collective Responsibility! Linapokuja suala la collective responsibility, kama jambo hukubaliani nalo unatakiwa kujiuzulu ili hatimae uwe na uhuru wa kuzungumza ni kwanini hakubaliani nalo!!
Na kwavile hapa tunazungumzia Spika/Mbunge, wala hakuwa na sababu ya kujiuzulu ulu ateme nyongo kwa sababu tayari Ibara ya 100(2) inampa uhuru wa kuongea chochote
ndani ya bunge bila kuingiliwa na bila ya kuingiliwa na mamlaka yoyote provided analoongea lisiwe linakiuka sheria zingine!!
Sasa kama taasisi anayoongoza Ndugai ilishakubaliana na kupitisha bajeti iliyotaja suala la kukopa, huwezi tena kutoka nje na kuponda jambo lile lile uliloshiriki kuidhinisha, tena mara nyingi kwa mbwembwe na tambo!!!
Tena afadhali angekuwa mbunge wa kawaida, lakini Spika!! Tena Spika aliyepata uspika kwa mgongo wa chama kile kile!!