Dhana ya kwamba mshahara ukiongezwa na inflation itatokea ni dhana inayopaswa kufikiriwa na kichaa tu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Ninasema kuwa dhana hii ni mfu kwa sababu zifuatazo;

1. Je, kwa miaka 5 ya Magufuli bei za vifaa vya ujenzi iko palepale Kwakuwa mshahara haujaongezwa?.

2. Je, Tangu tupate uhuru mpaka sasa Marais waliopita ndio walichangia kuongezeka kwa bei za bidhaa kwa kuruhusu ongezeko la mshahara kwa watumishi?.

3. Mbona wabunge wanalipwa pesa nyingi kuliko watumishi wa umma ?. Kama kiasi cha pesa anacholipwa mtendaji wa mtaa ni sawa na hakipaswi kuongezeka ili kukwepa inflation, je kwanini wabunge nao wasilipwe kwa figure sawa na huyu mtendaji wa mtaa . Si mnasema kinatosha .

4. Je, mshahara wa mtumishi wa umma wa ngazi ya kawaida ( sio kiongozi) unatosha kupata mahitaji yake yote muhimu ?.
Haya mawazo ya kutokuwaongezea watumishi mishahara kisa inflation ni ya kipumbavu na hayapaswi kufikiriwa na mtu mwenye utu na akili timamu.

Mtu analipwa zaidi ya milioni kumi halafu anakuja kutoa mawazo mfu namna hii huku akisahau kuwa kuna watu take home yao ni 400,000 au pungufu.
 
Matatizo yaliyopo nchini ni makubwa kuliko wstumishi kuongezewa mshahara. Watumishi hawafii hata 1% ya watanzania wote. Ukiweka wategemezi wao hata useme kila mmoja ni 20 bado haifiki hata robo ya watanzania.
Hivyo hili kundi kubwa watanzania wanalotegemea na ambalo Lina 75% ya watanzania wote ndio la kufikiriwa sana
 
nani kaongea kauli hii?
 
Wewe akili yako imeghoshiwa sio bure.
Unajua mtumishi wa umma ndiye anayepaswa kutatua matatizo hayo uliyoyataja. Na mshahara ndio source kuu ya mapato yake . Unavyoleta blabla za kiabunuasi unakuwa hueleweki.
 
nani kaongea kauli hii?
Wapuuzi wengi tu huongea hili hata humu jf . Mada yoyote ikigusa maslahi ya Watumishi tu wanakuja na huo upuuzi wao wa inflation.
Bahati mbaya wengine ni viongozi wa serikali wanalipwa pesa ndefu na kupewa mahitaji yao yote muhimu bure.
 
Hasa kichaa yule wa chato ambaye amenyakuliwa mawinguni, wakati yeye alikua anahonga hadi ukuu wa wilaya na ukurugenzi ili wapate maslahi lakini kwa wengine alikua anaona kuwaongezea mshahara ni anasa rot in hell
 
Kuna vitu hapa Tz vibadilishwe haswa haswa hawa viongozi wetu(sijui wanawaza kwa kutumia nini)wanatoa hoja za ajabu ajabu......sasa haumpandishi mtu mshahara kwa miaka 7 unategemea nn
 
Kama wewe sio kichaa nijibu hili swali; Je, mnataka muongezewe mishahara, kwani mmeongezewa kazi?
Kwanini badala yake msidai serikali iboreshe mazingira ya uzalishaji mali na huduma ili bei za bidhaa zishuke? Mfano ukishusha bei ya umeme maana yake uzalishaji wa bidhaa utakuwa na tija zaidi na bei za bidhaa zitashuka. Ndio maana nasema abarikiwe alieanzisha mchakato wa bwawa la Rufiji, lile bwawa ndio mwarobaini wa matatizo kama haya
 
Wapuuzi wengi tu huongea hili hata humu jf . Mada yoyote ikigusa maslahi ya Watumishi tu wanakuja na huo upuuzi wao wa inflation.
Bahati mbaya wengine ni viongozi wa serikali wanalipwa pesa ndefu na kupewa mahitaji yao yote muhimu bure.
Mpuuzi mwenyewe
 
Siku zote nilikuweka kwenye kundi la watu wenye akili! Kumbe nilikuwa niko wrong kwa 100%

Aibu naona mimi. 🤔
 
Sasa ndiyo umeandika nini!! Watu kama nyinyi hamkustahili kabisa kuzaliwa kama binadamu! Bora ungekuwa Kenge tu.
 
Kuna vitu hapa Tz vibadilishwe haswa haswa hawa viongozi wetu(sijui wanawaza kwa kutumia nini)wanatoa hoja za ajabu ajabu......sasa haumpandishi mtu mshahara kwa miaka 7 unategemea nn
Hatuongezi mishahara kwa sababu hatujawaongezea kazi; badala yake tunampango wa kushusha bei za bidhaa kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma wenye tija kupitia mipango mkakati kama Rufiji na SGR.
 
Kwanini usijibu hoja kwa hoja?
Tatizo huna hoja! Mfanyakazi hana tofauti na wewe hapo unapodai au kupigania haki zako! Mfano haki ya kuishi, kuongea, kuabudu, nk.

Mfanyakazi kudai stahiki zake kutoka kwa Mwajiri, siyo dhambi. Ni jambo la kawaida duniani kote. Na hakuna uhusiano kati ya haki za wafanyakazi, na huo uouuzi ulio usema.

Yule kichaa wenu aliwaharibu sana akili. Na ndiyo maana Muumba alimchukua mapema ili kuwaokoa kuwa wendawazimu kabisa. Eti siwezi kupandisha mishahara, kwa sababu nanunua ndege kwanza!!

Sasa kuna uhusiano gani kati ya mshahara wa mfanyakazi na kununua ndege!
 
Hatuongezi mishahara kwa sababu hatujawaongezea kazi; badala yake tunampango wa kushusha bei za bidhaa kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma wenye tija kupitia mipango mkakati kama Rufiji na SGR.
Una akili kama Ndugai! Hovyo kabisa.
 
Hatuongezi mishahara kwa sababu hatujawaongezea kazi; badala yake tunampango wa kushusha bei za bidhaa kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma wenye tija kupitia mipango mkakati kama Rufiji na SGR.
Kwa hili uliloandika unamdhalilisha huyo kwenye avatar yako....!!

Mnachojua ni maslahi yenu binafsi na matumbo yetu SGR maana ake nn ili hali watu wanalia na ugumu wa maisha...yule aliyeanza kazi 2014 akiwa hana familia leo hii ana familia na wategemezi kibao halafu unamlipa kiasi kile kile.....akidai haki yake mnampa visingizio kibao na mwisho wa picha mnawaambia kama hawataki kazi waache.....dah...siku nikimiliki bunduki nitafyatua ubongo wa watu wengi😊🍺🍺🍺
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…