Dhana ya kwamba mshahara ukiongezwa na inflation itatokea ni dhana inayopaswa kufikiriwa na kichaa tu

Umemjibu kitaalamu.
Hongera
 
Reactions: Tlg
Mwambie tu, usipoongeza wanaoajiriwa=kuwaongezea majukumu walio ndani ya ajira.
 
Acha kujidanganya wewe

Anayelipwa mshahara gross 720,000 Na MTU analipwa mshahara 3.8m jumlisha posho 11 m hawawezi fanana


Wa laki saba atajenga nyumba baada ya miaka mingapi Huyo? Atasomesha wanae shule za aina gani? Atakula chakula cha aina gani? Ataweza kununua usafiri binafsi baada ya miaka mingapi?

Atamalizaje deni la loan board(Heslb) kwa mshahara huo?

Unachosema ni kufurahisha genge tu hapa

Mshahara mkubwa = maendeleo ya haraka ,Maisha bora zaidi.

Mwalimu ata u budget mshahara vizuri kiasi gani huwezi shindana Na gavana wa benki kuu kimaendeleo kwa mshahara tu au mbunge au wakurugenzi was mashirika hawa.
 
We hujui mzunguko wa pesa ukiwa mkubwa uliyejiajiri unafaidika pia !??
 
Alichokizungumza hapa kinaweza kuzungumwa na motivational speaker tu
Ni ujuha kabisa.
Kwahiyo wabunge wote Wana gari za maana inamaana wanajua sana kupangia bajeti mshahara wao tofauti na Askari magereza?
 
Halafu pengine una mavyeti na kujiita msomi.
Hivi nyanya unayonunua wewe mwenye mshahara wa ml 3.8? Nyanya yako inalimwa kwenye mawe? Huyo mwenye mshahara wa laki 7 yeye nyanya anayonunua inalimwa kwenye mapango?
Bei ya mafuta ukienda sheli huwa unaulizwa unapokea kiasi gani ili upangiwe Bei? Au Bei huwa Ni kwa Wote?

Fikiria Tena kabla ya kuandika upuuzi.

Kujiongeza majukumu ni maamuzi yako, Bei za sokoni zikibadilika huathiri zaidi wenye kipato Cha chini,maana hawatoweza kukidhi mahitaji yao.
 
Alichokizungumza hapa kinaweza kuzungumwa na motivational speaker tu
Ni ujuha kabisa.
Kwahiyo wabunge wote Wana gari za maana inamaana wanajua sana kupangia bajeti mshahara wao tofauti na Askari magereza?
Acha tu Mkuu kuna watu wanamawazo ya ajabu sana. Motivational speakers ndo huwa wanakauli kama hizo sure!! Huku wao wakikusanya viingilio [emoji23][emoji23][emoji23].



Eti mshahara ukipanda Na mahitaji yako yatapanda so hamna tofauti!!!

Kupanda kwa mahitaji ndo ubora wa maisha umeongezeka huwezi lipwa 10m ukala ugali mchicha mkavu kila siku!! Utaanza kuchanganya samaki, kuku Na udambwidambwi mwengine

Huwezi pigania daladala kuingia dirishani utanunua usafiri wako mzuri wa luxury tu kama hapo tofauti haionekani basi unaugonjwa wa akili.
 
Bidhaa gani itashuka ambayo imepanda kuanzia 2016?
 
Hayo ndio mabadiliko Sasa kupitia mshahara.
Ndio kumove from one stage to another stage of life (maendeleo)

Halafu bado Kuna mapuuzi yanasema mshahara hauwezi kutosha.
Hata usipotosha,si umeshapata maendeleo? Bora ustoshe lakini tayari umeendelea.
 
Ni kwanini usijibu hoja kwa hoja?
.
 
Kuongeza fedha bila kuongeza uzalishaji si ndio inflation tunayozungumzia hapa?
 
Wakati wa Corona mwaka jana bei ya pipa la mafuta ilikuwa dola 38. Je huku kwetu kuna nauli ya daladala ilishuka?
Usitegemee umeme wa Rufiji utashusha bei ya bidhaa yeyote sana sana utapunguza bei ya unit tu.
Haya sasa ndio ya kulalamikia na kuyadai
 
Hayo ndio ya kudai, serikali iajiri watumishi wa kutosha kulingana na mahitaji. Wengi bado wanatafuta ajira. Na pia bei za bidhaa zishuke kwa kuongeza uzalishaji wenye tija.
 
Injection kubwa ya pesa katika mzunguko bila kuongeza uzalishaji wenye tija? Unajua nini kitafuata
Ukifanya importation hupati hizo bidhaa ili kuweka ratio ya mzunguko wa pesa? Sio lazima uzalishe wewe. Wewe kazi yako Ni kuhakikisha demand inakuwa kubwa tu ili wafanyabiashara wakulipe Kodi
 
Ukifanya importation hupati hizo bidhaa ili kuweka ratio ya mzunguko wa pesa? Sio lazima uzalishe wewe. Wewe kazi yako Ni kuhakikisha demand inakuwa kubwa tu ili wafanyabiashara wakulipe Kodi
Hiyo importation unafanya kwa shillingi au Dollar? Shillingi nyingi zikikimbiza Dollar chache katika exchange ili kufanya importation, unajua kitakachofuata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…