kt the irreplaceable
JF-Expert Member
- Oct 12, 2017
- 2,375
- 4,893
Nimewasikia baadhi ya wanachama wa yanga wakiunga mkono hoja iliyotolewa na billionaire Rostam Aziz akiwashauri timu ya yanga inapaswa kubaki na mfumo wa wanachama badala ya kampuni, nimebaki najiuliza hivi yanga wanajua wanachokitaka kweli?, wana uelewa wowote juu klabu kujiendesha kiuchumi?
Yanga toka izaliwe inajiendesha kwa mtindo wa wanachama lakini mpaka leo ni omba omba, mpaka leo wachezaji wanagoma kisa mishahara... mpaka leo hawewezi kujitegemea.
Hawajiulizi kwanini matajiri kama Manji, Mengi, Gulamali nk waliifadhili Yanga lakini mpaka leo timu ni maskini kachoka? Hawajiulizi hao matajiri wananufaikaje na jina la yanga?
Kwenye dunia ya leo ya modern capitalism (imperialism) wenye mitaji ndo wenye mamlaka. Tanzania tunalilia wawekezaji kila siku, kwanini hatujifunzi? Simba ilipita miaka sita wamepoteana, pesa za mo zimeleta utulivu.
Yanga wanapaswa kumuangalia kwa jicho la tatu Rostam Azizi. Hyo milioni 200 aliotoa siyo ya bure. Wanauchumi husema "hakuna chakula cha bure kwenye uchumi wa kibepari" (no free lunch in capitalist economy) kwasababu anatoa msaada atakua na sauti, kama ilivyokua kwa manji.
Tukubali tukatae, wanachama wa yanga akina akilimali hawana pesa, hata pesa ya kubadili nguo kwao ni shida wataweza kuimiliki yanga? Unaimiliki timu kwa kutegemea kuomba? Yaani unafuga mbwa kwa kutegemea mavi ya walevi?
Akili ni nywele na kila mtu ana zake