Dhana ya mabadiliko ndani ya Yanga, wanajua wanachokitaka??

kt the irreplaceable

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2017
Posts
2,375
Reaction score
4,893
Nimewasikia baadhi ya wanachama wa yanga wakiunga mkono hoja iliyotolewa na billionaire Rostam Aziz akiwashauri timu ya yanga inapaswa kubaki na mfumo wa wanachama badala ya kampuni, nimebaki najiuliza hivi yanga wanajua wanachokitaka kweli?, wana uelewa wowote juu klabu kujiendesha kiuchumi?

Yanga toka izaliwe inajiendesha kwa mtindo wa wanachama lakini mpaka leo ni omba omba, mpaka leo wachezaji wanagoma kisa mishahara... mpaka leo hawewezi kujitegemea.

Hawajiulizi kwanini matajiri kama Manji, Mengi, Gulamali nk waliifadhili Yanga lakini mpaka leo timu ni maskini kachoka? Hawajiulizi hao matajiri wananufaikaje na jina la yanga?

Kwenye dunia ya leo ya modern capitalism (imperialism) wenye mitaji ndo wenye mamlaka. Tanzania tunalilia wawekezaji kila siku, kwanini hatujifunzi? Simba ilipita miaka sita wamepoteana, pesa za mo zimeleta utulivu.

Yanga wanapaswa kumuangalia kwa jicho la tatu Rostam Azizi. Hyo milioni 200 aliotoa siyo ya bure. Wanauchumi husema "hakuna chakula cha bure kwenye uchumi wa kibepari" (no free lunch in capitalist economy) kwasababu anatoa msaada atakua na sauti, kama ilivyokua kwa manji.

Tukubali tukatae, wanachama wa yanga akina akilimali hawana pesa, hata pesa ya kubadili nguo kwao ni shida wataweza kuimiliki yanga? Unaimiliki timu kwa kutegemea kuomba? Yaani unafuga mbwa kwa kutegemea mavi ya walevi?

Akili ni nywele na kila mtu ana zake
 
Hii ya michango ni danganya toto tu yanga kuna wafadhili wanamwaga hela ndefu mule na hawataki kujulikana
 
kwa hiyo unataka yanga imilikiwe na mtu mmoja kama simba.? rostam alichosema ni timu ipate makampuni ya kudhamin kama wanavyofanya barcelona na real madrid, sio kuimilikisha kwa mtu mmoja siku akiondoka timu inayumba
 
Psg, Liverpool. Man City, Tp Mazembe Ni baadhi ya Vilabu Vinavyomilikiwa na watu na Bado Timu Inapata Makapuni ya Kuvidhamini na Vina Mafanikio Makubwa,.

Ipo Siku Watu Watachoka Kuichangia,. Kazi ya Shabiki ni kuishangilia Timu Na Kuona ina Mafanikio haijalishi Inamilikiwa na Nani..
 
Robidinyo Barcelona Na Real Madrid zinamilikiwa na wanachama na zinafanya vizuri. Yanga ina wanachama zaidi ya milioni 3 hawawezi wote kuchoka kuichangia, hata kila mwezi wakifanya harambee watu wa kuichangia watakuwepo, tofauti na simba mo biashara zake zikimuendea vibaya akajitoa na simba imekufa, kumbuka mo alivyotekwa simba walivyohaha kila siku kusoma dua
 
Rostam alisema mfumo wa wanachama urekebishwe halafu timu zitafute mwekezaji mwenye maslhi mapana.pia timu iendeshwe kwa kisasa kwa mifumo ya uongozi imara bila kuipeleka timu kuwabya mtu 1.Mi pia anakubariana nae 95%
 
Tatizo watani akili zao wamekabidhi na Mo,kauli kama hii aliitoa JK siku ya kuchangia Yanga jana Rostam Azizi karudia kwa mapana lkn hawaelewi....
Pilipili ya shamba yawawashia nn? Tulieni tukutane kiwanjani.
Kumuelewa Rostam inataka akili kubwa.
 
wakina Rostam ni watu walochafuka kwa jamii na kuchukiwa na kila mtu njia pekee ya kusafisha majina yao ni kujiingiza kwenye ufadhili wa mpira sasa huoni mtu akimzungumzia Rostam kwa mabaya bali ni jinsi gani anavyotaka kuisaidia yanga bahati mbaya wasingeweza kwenda simba maana tayari simba wana mtu wao wameichagua yanga kwa sababu hakuna kipindi yanga inahitaji fedha kama kipindi hichi
 
kwa hiyo unataka yanga imilikiwe na mtu mmoja kama simba.? rostam alichosema ni timu ipate makampuni ya kudhamin kama wanavyofanya barcelona na real madrid, sio kuimilikisha kwa mtu mmoja siku akiondoka timu inayumba
Kwanini miaka yote wanashindwa kupata hayo makampuni?
 
Rostam alisema mfumo wa wanachama urekebishwe halafu timu zitafute mwekezaji mwenye maslhi mapana.pia timu iendeshwe kwa kisasa kwa mifumo ya uongozi imara bila kuipeleka timu kuwabya mtu 1.Mi pia anakubariana nae 95%
Huyo mwekezaji ndo mmiliki mwenyewe.... atachofanya atawekeza labda bilion 5 kwa hisa za asilimia 25. Umiliki si lazima uchukue kampuni nzima. Unaweza kumili sehem ya timu. Hii kitu haipingiki
 
Wakitoa milion 200 watu wanapapatika wanashindwa kujua yanga ina thamani zaidi ya hiyo.
wakina Rostam ni watu walochafuka kwa jamii na kuchukiwa na kila mtu njia pekee ya kusafisha majina yao ni kujiingiza kwenye ufadhili wa mpira sasa huoni mtu akimzungumzia Rostam kwa mabaya bali ni jinsi gani anavyotaka kuisaidia yanga bahati mbaya wasingeweza kwenda simba maana tayari simba wana mtu wao wameichagua yanga kwa sababu hakuna kipindi yanga inahitaji fedha kama kipindi hichi
 
Huyo mwekezaji ndo mmiliki mwenyewe.... atachofanya atawekeza labda bilion 5 kwa hisa za asilimia 25. Umiliki si lazima uchukue kampuni nzima. Unaweza kumili sehem ya timu. Hii kitu haipingiki
Upo sahihi.lakin hii inaleta mwanya wa makampuni mengine kuwekeza bila shida.mfano yanga kuna uweEkano wa kuachana na sportpesa wakatafuta kampunni nyingine.
YANGA inapaswa kuwa hata na wadhamini katka jezi tu hata 3 wenye kuweka nembo zao hiyo tu ni zaidi ya bil 10.mfano ukichukua Voda,mbele ya jezi,kwenye mikono mihan gas,mgongoni chini inakaa Dangote cement.mkataba usizidi miaka 3.Hapo mnahakikisha jezi zote zipo za bei kubwa na bei ndogo.

Pia mnaweza kujenga uwanja mdogo tu kama ule wa azam complex.uwanja anapewa kampuni jina lake kwa muda wa miaka 10.mfamo unaingia mkataba na kampuni ya azania.inakuwa Azania stadium.Ofisi za Yanga zihamishwe hata eneo lingine tofauti na jangwani halafu jengo liwe la kitegauchumi. Jengo pekee kodi yake kwa mwezi itaingiza kama mil400.n.k.mnatafuta kampuni uarabuni wanatengezeza vifaa kama vile saa,kacha,opena na vitu vingivinaingiza mil.150 kwa mwezi.Hapo mnatafuta kampuni ya maji itakayotumia nembo zenu inaingiza mil.20 kwa mwezi.

Baada ya mwaka klabu inakusanya Bil 120.Baada ya miaka 10.klabu inaingiza Bil 800.Hayo yote ni ikiwa kutakuwa na usimamizi mzuri na watu wajitambue
 
Waache wapambane na hali zao, rostam anajua anacheza mchezo gani, "kumpumbaza mkulu"
 
Sina la kuongeza mkuu, wenye macho na waone
 
Rostam! Rostam Aziz ni zaidi ya akili. kwa muonekano nikama mtu fulani mzembemzembe hivi, hata akiongeo maneno yake hatyatiliki maanani, kuna gazeti moja nakumbuka kama sio mwanahalisi liliwahi sema Rostam ni kama kanisa Katoliki. mambo anayofanya leo yanakuwa na impact baada ya miaka kadhaa mbeleni na mara zote hajawahi tenda jambo kijinga bali mara zote hutenda kwa kutaraja faida!! yanga wameanza kuchangishana toka zamani na wamewahi kuwa na wadhamini wengi tuu lkn hakuna linalobadilika. ok tufanye hivi ''yetu macho na siku hazigandi tuombe uzima.............''
 
Back
Top Bottom