Mbogo nyeusi
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 233
- 541
Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo mh rais aliapa kuilinda inatoa nafasi ya vyama vyote kufanya mikutano ya hadhara kuzungumza na wanachama wao.
Kauli ya mama ya kwamba mikutano ya hadhara kwa sasa hapana na inaruhusiwa kwa mbunge au diwani afanyie Jimboni kwake inasikitisha na pia inakanyaga katiba ,kumbe hakuna umuhimu wa kuwa na katiba Kama mtu anaweza akadharau katiba aliyo apa kuilinda,hilo katazo linasimamia kifungu gani Cha katiba?
Vyama vya upinzani wiliporwa ushindi kwenye uchaguzi hawana madiwani,wabunge na hata wenyeviti wa mitaa,je vyama hivyo vinaweza vipi kukutana na wanachama wao ikiwa hawana wawakilishi kwenye hizo nafasi?
Na ukisema watafanya mikutano ya ndani ni ukumbi gani unaweza kubeba wafusi wa chama wa kataa nzima kwa mara moja?haiwezekani vyama vingine wao wasifanye mikutano ya hadhara kwamba wanaruhusiwa mikutano ya ndani wengine wao wanaruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara,kwa kuwa katazo siyo la leo tulioana serikali ya awamu ya tano ambapo Dr Bashiru, Polepole na Hery James walizunguka nchi nzima,katazo lile lile limejirudia kwa style ile ile ya kujenga uchumi wa nchi.
Mwanasiasa kazi yake ni kufanya siasa,Kama hakuna mikutano siasa ataifanyia wapi?
Vyama vyote makini vina viongozi kuanzia ngazi za vijiji na vitongoji na yupo mtu wa uenezi wa chama,huyo mwenezi anaenezaje itikadi za chama ikiwa haruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara?
Katazo hili lisingeleta ukakasi Kama chama tawala nao wangekaa bila kufanya hiyo mikutano,awamu iliyopita walizunguka wenyewe nchi nzima wakieneza Tanzania ya kijani hakika ni aibu.
Mh rais nakushauri katika hili rudi kwenye katiba uliyo apa kusimamia, ccm wapo makada wazuri hofu iko wapi kujibu mashambulizi?
Waache wanasiasa wafanye siasa kwa kufata katiba yetu hiyo ndio kazi yao,
Ondoa haya manunguniko uchumi hauwezi ukazuiwa kwa mkutano utakaofanyika furahisha wa masaa mawili,na pia hayupo wa kukuzuia kufanya maendeleo kisa mikutano,mzee wetu Kikweta alishindwa kuleta maendeleo kisa mikutano ya siasa?acha uoga wakina nape wapo kujibu hoja za wapinzani.
Nashauri mikutano ya hadhara iruhusiwe kwa vile wapinzani hawana wawakilishi majimboni kwa level zote kuanzia mwenyekiti wa mitaa,diwani na mbunge nchi nzima,hivyo kwa kutumia kigezo hicho unawanyima haki ambayo ipo kikatiba.