Dhana ya "plea bargaining" itoe mwanga Marekani inaweza kufanya nini kuhusu waasi magaidi wa Syria

Dhana ya "plea bargaining" itoe mwanga Marekani inaweza kufanya nini kuhusu waasi magaidi wa Syria

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kwenye mifumo mingi ya sheria ya Magharibi kuna kitu kinaitwa "Plea Bargaining" . Kwenye huu mfumo ni kwamba muendesha mashitaka anatengeneza dili kwa mshitakiwa kushirikiana naye kumpa taarifa muhimu kwa ajili ya kufanikisha lengo kubwa zaidi kwa faida ya mshitakiwa kupungiziwa adhabu, kuachiliwa kabisa au hata kupewa ulinzi maalumu.

Wakati Marekani inapambana na Mafia miaka hiyo wanasumbua sana Marekani waendesha mashitaka walitumia sana plea Bargaining. Kwenye operations za dawa za kulevya zinafanyika plea bargains na hata pia kupambana na magaidi kunafanyika plea bargains.

Yani kuna magaidi huwa wanagundilika au wanakamatwa kisha wanaingia katika makubaliano na FBI, CIA na wanasheria wa serikali kuwapa taarifa za kufanikisha malengo makubwa zaidi kisha wanaachwa wanarudi mtaani kuendelea na maisha yao.

Waasi wa Syria wa HTS na wengineo sasa hivi waliomuondoa Assad kama wanaweza kuiambia Marekani wanaachana na ugaidi na watakuwa washirika wazuri dhidi ya Iran na Hezbollah sioni sababu za zitakazoifanya Marekani iendelee kupambana nao au kuwawinda.

Nimemsikia Mohammed al Jolani kiongozi wa HTS akitubu kwa kauli mbalimbali kwamba hajawahi kufanya mauaji alipokuwa katika mrengo wa ugaidi, kwamba watu wanabadilika wanavyowaza wakiwa na miaka 20, ni tofauti na wakiwa na miaka 30, ni tofauti wakiwa na miaka 40 na pia ni tofauti wakiwa na miaka 50 na kuendelea. Anasema haikubaliani na wenye msimamo mkali wa kidini!

Pia amesema makundi yote ya dini Syria yataishi kwa amani, uhuri na haki zao kuzingatiwa kwani wamekuwepo Syria kwa zaidi mamia ya miaka. Huenda ni ahadi hewa pia kwa ajili ya kukamata na kudhibiti madaraka kikamilifu lakini katika harakati zao za kujisafisha mpaka sasa "so far so good".
 
Back
Top Bottom