Dhana ya PPP inapotoshwa sana na kina kafulila na serikali haiwezi kwepa majukumu yake kwa kivuli cha PPP

Dhana ya PPP inapotoshwa sana na kina kafulila na serikali haiwezi kwepa majukumu yake kwa kivuli cha PPP

Mpigania uhuru wa pili

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2023
Posts
3,380
Reaction score
6,376
Kuna miradi ni jukumu la serikali kuibeba hasa ile inayohusu kuhudumia wananchi mfano barabara, hospitali, kusambaza umeme, maji na mingine kama hiyo hiyo ni jukumu la serikali kuitekeleza

Kuna miradi kweli unahitaji PPP kuitekeleza sababu utekelezaji wake unahitaji fedha kubwa mfano
  • Mradi wa kuchakata gesi asilia Lindi unahitaji mwekezaji sababu gharama yake ni kubwa sana usd billion 40 ni kubwa sana
  • Mradi wa kujenga oil refinery sababu unahitaji mtaji mkubwa
  • Mradi wa kujenga petrochemical plant unahitaji mtaji mkubwa
Kuna miradi inahitaji mitaji mikubwa ila ni vizuri ikifanya na serikali
  • Mradi wa bandari kutokana na umuhimu wake ni vizuri ukawa chini ya serikali
  • Mradi wa treni za umeme ni vizuri ukawa chini ya serikali
Nachokiona ni dhana ya PPP inapotoshwa sana ni kama serikali inataka kukumbia majukumu yake ya msingi na kutumia PPP kama shortcut

Mfano mdogo tu daraja la kigamboni yale ndo matokeo ya kutumia PPP hadi kwenye maeneo ambayo hayatakiwa matokeo yake wananchi wanalipishwa fedha kutumia lile daraja

Jana Rais anasema wanatafuta mwekezaji ajenge barabara ya handeni mpaka singida unajua ni kichekesho matokeo yake yatatokea kama yale yale ya daraja la kigamboni

Kama serikali inataka kila jambo kuwatupia PPP wao kazi yao ni nini hasa mbona tuna-viongozi wavivu sana wasiotaka kuwajibika ilihali wanalipwa mamilion kila mwezi
 
Hapo ndio Magufuli atakumbukwa.

Viongozi wetu ni waoga.

Magufuli asingeingia madarakani

hiyo miradi mikubwa alianzisha ingebaki kuwa ndoto.

Kuna baadhi ya maamuzi unafanya unafumba macho bila woga, ila viongozi wengi ni waoga na wanakwepa changamoto kwa kusingizia kukosa fedha.

Ni sawa na mtu unataka kujenga nyumba, gharama umeambiwa mpaka ikamilike ni 120m, na ukijiangalia na kujtathmini unaona kabisa hauna hiyo 120m, kwa hiyo kwa uzwazwa utaendelea kumgoja mpaka upate hiyo 120m ndio uanze ujenzi hizi ndio akili za viongozi wetu. Wakati unaweza anza na 20m kama nia na lengo lipo.

Bado nampa heko nyingi Magufuli, mpaka leo tungekua tunategemea mitambo ya gas na ile ya wale matapeli wa marekani.

Usipokua na maamuzi magumu hamna cha maana utafanya.
 
Bora ikwepe hayo majukumu Kisha ifanye mambo mengine, mfano ajira kwa vijana wa Tanzania haziongezwi, health facilities hazieleweki, kwa sehemu kubwa watu wa Hali ya chini ( ambapo ni wengi )wanazidi kuchanganyikiwa na wengine kukata tamaa.😭😭
 
PPP ni Ukoloni mamboleo tu.

Hizo fedha mahali popote kule zinapotokea, ni Serikali inayotoa guarantees na ni serikali hio hio yetu na Wananchi ndio wataenda kubeba zigo la madeni na matozo. Faida zinarudi huko kwa hao wanajiita Private Investors, jina lingine tu la wakoloni.

Tunawawezesha wageni badala ya wazawa/wenyeji.

Huo kwa mtazamo wa wataalam wengi na wangu ni Ukoloni mamboleo tu.
 
Tena ukute hapo sector binafsi mitaji Yao ni fedha hizo hizo za wananchi. Walizozipata wanavuojua wao na wanaoshirikiana.

Na ppp ndio ukawa mbadala wa kuficha pesa benk za uswiss ama visiwa fulani kama ilivyo kwa viongozi wengi wa kiafrica.
 
Tena ukute hapo sector binafsi mitaji Yao ni fedha hizo hizo za wananchi. Walizozipata wanavuojua wao na wanaoshirikiana.
Hii mipango ya PPP itatuacha kuwa dependent na hizo fedha na kila kitu kingine. Kama hii misada inavyotuacha sasa. Vulnerable.

na ikitokea tuuwaletee mbinde kidogo (pandisha tozo n.k)utaona.

yani uone Wb IMF na serikali zao zitakavyokuja juu. Yale yale, kabla na wakati wa ukoloni.

Tambua ni makampuni ya ulaya ndio yalikuwa yakifanya biashara kabla ya serikali zao kuingilia.

wakapewa baraka na bunduki na serikali zao pale Waafrica walivyaanza kuresist unyonyaji

Haitakuwa tofauti safari hii. Tuna kina mangungu wapya .
Na ppp ndio ukawa mbadala wa kuficha pesa benk za uswiss ama visiwa fulani kama ilivyo kwa viongozi wengi wa kiafrica.
Haswa. Mie naona ni kama legalisation tu ya fedha kurudi nje. IFF's

Upo sahihi.
 
Back
Top Bottom