Dhana ya uhaba wa wanaume: huwaweka baadhi ya wanawake katika mahusiano magumu…!

Dhana ya uhaba wa wanaume: huwaweka baadhi ya wanawake katika mahusiano magumu…!

Kuna wanaomudu kutoka kwenye uhusiano wa aina hiyo, hawa ni wale ambao wanajua nini maana ya kupenda wao hawasukumwi na mihemko, bali husukumwa na kupenda. Kwao msamiati kwamba wanaume ni wachache au hakuna wanaume wa kuoa haupo kabisa akilini mwao..............

Kaka naungana na wewe, kuna ukweli kuwa wako wanawake wanaong'ang'ania kwenye mahusiano kwa hofu ya "wanaume ni wachache" Lakini wingi au uchache wa watu ni sababu tosha ya kumfanya mtu aishi kwenye hali ya dhiki, mateso na majuto? Je mwanamke hawezi kuishi bila mwanaume? Kuna sababu gani ya kuishi kwenye ndoa ya mateso?
Nafikiria inatakiwa wanawake wafikie kipindi wajiamini na kuondoka na dhana potofu ya kuwa wanaume ni wachache na hivyo wanatakiwa kung'ang'ania hata kama wanapata mateso ya namna gani.
 
Uzi wako umenikumbusha sura za watu tofauti niliokutana nao katika maisha wengine ni wa karibu yangu kabisa. Wanaishi katika ndoa hizi wakitegemea kuwa kuna siku mwanaume huyo atabadilika and roughly is about 10 yrs and this person has never changed.

Jamii ni mojawapo ya mwanamke kudhalilika, pili ni kufikiria watoto hasa wakiwa wadogo hakuna mama anayetaka watoto wake wabeheneke ndio maana utakuta mtu anavumilia mateso yake yote kwa ajili ya watoto. Mbaya zaidi ikiwa mama mwenyewe si mwajiriwa au hana namna ya kuwa independent.

Mtambuzi , mimi naona kama tu umegusia hili tatizo lakini hebu tupe ushauri zaidi vipi mwanamke akabiliane na challenges kama hizi. Ikiwemo huo uhaba wa vidume....

JIBU HILI HAPA:

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/265908-badili-jiondoe-au-kubali-matokeo%85.html
 
Nadhani wanawake wengi pia wanalazimika kubaki kwenye mahusiano kwa sababu ya neno..'watu au jamii itanionaje'
Wakati mwingine makosa yaleyale ambayo yanavunja ndoa endapo yangefanywa na mwanamke yakitendwa na mwanaume jamii inachukulia poa..so, wanawake always wanajikuta wapo kwenye disadvantaged position!

kiongoz upo positive kabisa ningekupa like..ni simu tu..
 
Kuna swala la jamii itanionaje, lkn pia watoto wataishije na ile kitu famous ya 'mpaka kifo kiwatenganishe'.

Mengine ni kuamini kuna siku atabadilika, nitaanzaje maisha (uoga na of course nitampata wapi mwingine) na ujinga au kutojithamini sisi wenyewe wanawake!

Jamii has never been woman friendly hata siku moja. It is a big challenge to be a woman.

mrembo hata wewe akili ipo hapo kichwani mwako..hawa mods watuwekee like za simu...
 
na kitu ambacho wanawake wengi hawajui ni kwamba..wanawake ndio wanathamani kubwa sana na ndio adimu zaidi kuliko wanaume,maan kwa sasa ukisimamisha wanawake laki 1. wenye sifa na hadhi ya kuitwa wake ni elfu 8 mpaka10 .wengi hawafai hata kuwasogelea ..sasa wewe mwanamke mwenye moyo wa uvumilivu na sifa zote za kuwa mke hujioni ulivyo wa thaman na adimu?ni ukweli usiopingika kuwa wanaume hatuwezi kuishi na mwanamke asie na sifa za kuitwa mke..tena kama ukigundua huyu nimekosea kumuoa basi maamuziya kujitazama sasa huwa yanafuata..lakini kwa mwanamke mwenye sifa za kuitwa mke,kama unajitambua kuwa sifa hizo unazo usikubali kunyanyasika..wewe ni mtu mwenye thamani na inabidi ujijue ni gharama na bahati ya haliya juu mtu kuwa nawe kama mke.
 
Najua wanaume wataukimbia huu uzi kwa sababu nimewashika wanawake masikio....................LO

whisper.png

Angalia usiwashike sana wasije wakapata ajali

attachment.php
 
Mmmh kisu mfupani jamani.................ila na mateso ya wanawake wengine pia ni kama kuendeleza kiburi chao

Nimewahi kumsikia mmoja kuwa sitoki hapa labda atoke yeye ilhali ye ndo ana depression syndrome fully blown..............nilichanganyikiwa ila ulikuwa ndo msimamo wake

Msaada; Kama baba anamtesa mama au kumnyanyasa ni sawa kwa mama kuwaeleza watoto haswa kama ni watu wazima (watoto)?????

Mytake; Ni lazima mama kuwaelelza watoto ili wamjue baba yao na wajiunge kama timu katika kumrekebisha........mficha maradhi...............
 
Mtambuzi....leo nimebadilisha specs napata sana tabu jamani.........looh salaale uzee huuu balaaa
Ntasoma vizuri na kuchambia keshoooo....ona sasa.....aaah...ntachangia kesho!
 
Kuna swala la jamii itanionaje, lkn pia watoto wataishije na ile kitu famous ya 'mpaka kifo kiwatenganishe'.

Mengine ni kuamini kuna siku atabadilika, nitaanzaje maisha (uoga na of course nitampata wapi mwingine) na ujinga au kutojithamini sisi wenyewe wanawake!

Jamii has never been woman friendly hata siku moja. It is a big challenge to be a woman.

Hii comment yako imenitoa chozi kaunga,
 
Wanaume wanaojitambua na kujielewa ndio wachache kweli ila hiyo si sababu ya kung'ang'ania mahusiano yasiyo na furaha. Jamani wanawake tunaweza kuishi bila hawa wanyama wenye mikia mbele.
 
Looh mwanamke ukishagundua jamaa habadiriki kimbia kabisa, hapa kuna mazoea eti atabadilika hadi unazeekea pale na stress ndo zinauwa wanawake wengi.
 
Kuna swala la jamii itanionaje, lkn pia watoto wataishije na ile kitu famous ya 'mpaka kifo kiwatenganishe'.

Mengine ni kuamini kuna siku atabadilika, nitaanzaje maisha (uoga na of course nitampata wapi mwingine) na ujinga au kutojithamini sisi wenyewe wanawake!

Jamii has never been woman friendly hata siku moja. It is a big challenge to be a woman.

Asante nimeishaona point (in red) niliyotaka kuongezea
 
Wanaume wanaojitambua na kujielewa ndio wachache kweli ila hiyo si sababu ya kung'ang'ania mahusiano yasiyo na furaha. Jamani wanawake tunaweza kuishi bila hawa wanyama wenye mikia mbele.

Ukishafanya wrong choice ndo matokeo yake haya. Hii iko kote kote, kwa wanaume na kwa wanawake. Kuna wababa kibao tu nao wako kwenye mahusiano yasiyo na furaha
 
DUH................................Mtambuzi unamambo,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
Nadhani wanawake wengi pia wanalazimika kubaki kwenye mahusiano kwa sababu ya neno..'watu au jamii itanionaje'
Wakati mwingine makosa yaleyale ambayo yanavunja ndoa endapo yangefanywa na mwanamke yakitendwa na mwanaume jamii inachukulia poa..so, wanawake always wanajikuta wapo kwenye disadvantaged position!

SnowBall nimetafuta kitufe cha LIKE sikioni...................
Pokea LIKE yangu mkuu.

kwanza sijui nilikuwa wapi huu uzi ukanipita hivi ila b4 i proceed naomba nianze ku comment hapa.

si kweli kwamba wanawake tunang'ang'ania kwenye mahusianao yanayotuumiza eti kisa jamii itanionaje ama nitaishije la hasha. Mtambuzi na SnowBall jamani mnaish haa dunian mnajua mila za kiafrika zilivyo. Binti anapoposwa hadi akafanya ndoa somo kubwa analoambiwa ni akawe mtii na mvumilivu. kijana hana anachoambiwa zaid ya kamlee mkeo. sasa hali hii ukiirefer kwenye maandiko ya dini yanatufunga sana manake Mungu anasema alilolifunga yeyey mwanadamu asilitenganishe. hapa akina mama huwa tunabeba mzig wa je wanangu hawa nitawaambia nini kwamba nimedivarce na baba yao. je sitowajengea hatred kwa baba yao?

pia sisi akina mama huwa tunapenda pia kuyafikiria maisha katika wider angle. hivi wafikiri ni ngumu kuanzisha maisha mpya lkn unajifkiria nitakapo yaanza je wanangu wataish vipi?maskini ya mungu? ni ta coupe lakini wao watakubaliana na hali hi watayakubali maisha ? huwa hata siku moja hatufikirii ugumu wa maisa bali amani ya watoto basi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom