HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,567
Kuna wanaomudu kutoka kwenye uhusiano wa aina hiyo, hawa ni wale ambao wanajua nini maana ya kupenda wao hawasukumwi na mihemko, bali husukumwa na kupenda. Kwao msamiati kwamba wanaume ni wachache au hakuna wanaume wa kuoa haupo kabisa akilini mwao..............
Kaka naungana na wewe, kuna ukweli kuwa wako wanawake wanaong'ang'ania kwenye mahusiano kwa hofu ya "wanaume ni wachache" Lakini wingi au uchache wa watu ni sababu tosha ya kumfanya mtu aishi kwenye hali ya dhiki, mateso na majuto? Je mwanamke hawezi kuishi bila mwanaume? Kuna sababu gani ya kuishi kwenye ndoa ya mateso?
Nafikiria inatakiwa wanawake wafikie kipindi wajiamini na kuondoka na dhana potofu ya kuwa wanaume ni wachache na hivyo wanatakiwa kung'ang'ania hata kama wanapata mateso ya namna gani.