Dharau ilianza pale Hayati Magufuli alipokejeliwa ni Uchwara na Mshamba na CCM kukaa kimya

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ni vema tukaangalia tulijikwaa wapi na wala siyo tulipoangukia.

Siasa za matusi na dharau hazijaanza leo na hata kumkejeli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna awamu aliitwa Dhaifu tena bungeni na watu wakakaa kimya. Shujaa Magufuli aliitwa Dikteta Uchwara na huyu huyu ni yeye CCM ikapiga kimya. Shujaa Magufuli akaitwa Mshamba na yule Siasa Kali wa ACT Wazalendo, CCM kimya.

Leo mbegu ya kejeli na matusi ndio imeshakomaa, yaani kambale hukunjwa akiwa mbichi. Turudi kwa Viongozi wa Dini waturekebishie hili.

Heri ya Mwaka Mpya!
 
Yaani kuna wanasiasa wengine waliitwa "wezi kama kunguru". Hahaha!
 
Mimi sijaona tusi ,nani asiyejua Raisi anaakili ndogo hadi wanomtetea wanaona aibu ,
 
Kwani mtu kuambiwa ukweli ni kumtukana!
Mbona ni fair sentiments kabisa
 
Kutaja wasifu wa mtu siyo matusi.
 
Na huyo unayemuita shujaa naye aliwadharau wastaafu kwa kusema WANAWASHWAWASHWA..!!
 
Samia mwenyewe ni mtukanaji mzuri tu,alimuita Professor Mkenda nonsense hadharani. Tuvumiliane tu.
 
Tukuwekee hapa Matusi ya nguoni ambayo Nape alimtukana Lowassa ? Hii ya Lissu ni lugha kali ya kukemea haijawahi kuwa matusi , labda kama wewe ni mgeni
 
Wakati wanaccm wakimkebehi Lowassa kwa kashfa mbofumbofu za maradhi ulikuwa haujazaliwa?
 
Wakati wanaccm wakimkebehi Lowassa kwa kashfa mbofumbofu za maradhi ulikuwa haujazaliwa?
Chadema wakati wanamtukana Lowassa Kabla Mnyasa mwenzako Mbowe hajabadilisha Gia angani ulikuwa bado uko Malawi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…