Siungi mkono kutukanwa Rais wetu, yeye ni kama Nembo ya nchi! Panapotokea mtu akimtukana Rais, ni sawa na kusema, anaitukana Tanzanian na watu wake wote!
Hata hivyo, iko shida kubwa sasa katika jamii yetu, si viongozi na wasio viongozi
Huwenda Nchi yangu, watu wake wameathiriwa saana na ugonjwa wa kusahau, si vijana wala wazee
Labda tumuombe mheshimiwa Nape, asahihishe kauli yake kusema, Akitukanwa baba, wametukanwa mababa wote, hasa inapokuwa anatukanwa Rais
Yapo matusi yaliyokuwa akitukanwa hayati JPM, yaliwaumiza watanzania wengi na mimi nikiwemo, matusi yale yalienda mbaali sana hata kutaka kuitenga jamii ya wasukuma kwamba, ni watu wa hovyo na washamba washamba, ni kwa sababu tu Rais aliyekuwa akiongoza nchi alikuwa ni wa jamii hiyo!
Huko ni kupanda mbegu ya hovyo sana katika jamii yetu, na huwenda hata haya yanayotokea leo, chanzo chake ni hiyo mbegu iliyopandwa na wana ccm wenyewe!
Ifike wakati, kama taifa, tuseme kuna mahali tulikosea, kunyamazia dhihaka matusi na kejeli kubwa kabisa zilizokuwa zikimlenga Magufuli na jamii yake
Na kiongozi yeyote anaposimama kukemea udhalilishaji wa viongozi wetu, kwa kuwa kumbe ccm wameona ubaya wakutukanwa kwa viongozi, basi asisemee hili la leo peke yake, bali aanze kukemea yote yaliyokuwa yakiwadhalilisha viongozi wote wa kipindi cha nyuma miongoni mwao akiwapo hayati JPM
Niulize,
Wakati Hayati JPM akidhalilishwa, Nape hakuwepo? Aliwahi kukemea? Kama sio kuchochea moto?
Ccm, hiyo dhambi itawatafuna kwa kushindwa kuikemea
Mtasweka watu rumande na magereza yatajaa msijue chanzo ni nini?
Ni nyinyi chanzo cha hayo yote