SoC02 Dhibiti matumizi Yako!

SoC02 Dhibiti matumizi Yako!

Stories of Change - 2022 Competition

Kaaya10

Member
Joined
Dec 11, 2017
Posts
37
Reaction score
53
Ni Jambo la kushangaza, vipato vyetu ni tofauti na ukubwa wa familia na matumizi ni tofauti lakini mara nyingi sote hujikuta hatuna pesa au akiba. Kitu nnachojifunza hapo ni kua ukiamua kupunguza matumizi Yako na kuweka sehemu ya kipato Cha Akiba inawezekana kabisa kwani ukubwa au udogo wa familia, ukubwa au udogo wa kipato sio sababu ya kua na akiba.

Kuna aina mbili kuu za matumizi; matumizi ya lazima na Yale yasiyo ya lazima. Kila mtu ni wajibu wako kujifunza kujua yapi ni matumizi ya lazima na yapi sio matumizi ya lazima katika maisha Yako. Ukiyajua hayo ni rahisi kuhairisha baadhi ya mambo na kuweka hiyo pesa au Mali akiba.

Karibia Kila mtu ana mahitaji makubwa kuliko uwezo wake wa kuyatimiza.

Kama ambavyo magugu hukua shambani Kwa kupewa nafasi ndivyo na tabia ya matumizi mabaya huota na kukua na kuondoa kabisa uwezo wa kuweka Akiba.

Jambo la msingi, Hakikisha unaandika Kila kitu ambacho utahitaji kununua. Mali bila daftari hupotea bila habari. Hii inaitwa kuweka bajeti ya mapato Yako na matumizi. Lazima uwe unajua pesa zinakotokea na zinakoelekea Kwa afya njema ya Kifedha.

Kumbuka: Hata hayo mambo unayoyapenda huzuiliwi kuyaweka kwenye bajeti. Lengo la Bajeti sio kumbana mtu Bali ajue pesa zitakakotoka na kwenda.

Je unajua kuandaa bajeti? Kama Unahitaji msaada wa kuandaa bajeti binafsi au ya Biashara Njoo inbox


Kumbuael Kaaya | 0769160382
kaaya2012@gmail.com
 
Upvote 1
Back
Top Bottom