DOKEZO Dhulma inayofanywa na maafisa Uchaguzi wa Tume Huru ya Uchaguzi katika Jimbo Njombe Mjini kwa Waandikishaji wasaidizi na BVR

DOKEZO Dhulma inayofanywa na maafisa Uchaguzi wa Tume Huru ya Uchaguzi katika Jimbo Njombe Mjini kwa Waandikishaji wasaidizi na BVR

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Licha ya tangazo la mwaka 2024 la kutangaza nafasi za Kazi ya Muda ya waandikishaji wasaidizi na BVR OPERATORS kuaininsha malipo ya Kazi kuwa ni tsh 50,000 Kwa siku na yatalipwa Kwa siku zote za Kazi yaani siku Tisa pamoja na nauli ya kila siku tsh 10,000 Kwa siku zote Tisa za Kazi. Na ndivo ilivyolipwa Kwa baadhi ya mikoa ya Tanzania ambako ZOEZI limeshafanyika.

Kwa masikitiko makubwa Halmashauri ya MJI NJOMBE kinyume na tangazo la Tume Huru ya Uchaguzi maafisa wameamua kulipa tsh 5,000 Kama nauli tena kwa siku Saba badala ya 10,000 Kwa siku tisa kinyume na tangazo la tume huru ya uchaguzi. Pia FEDHA ya Kazi imelipwa kwa siku nne, licha ya Kazi kuelelea mwishoni tuna wasiwasi wa kuja kukatwa na fedha ya Kazi iliyobaki Kwa kuwa limekuwa ni Jambo la kawaida Kwa maafisa uchaguzi wa Jimbo hili la Njombe mjini. Hali inayopunguza morali ya Kazi Kwa waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya BAYOMETRIKI.

Jambo linalosikitisha Zaidi nikaambiwa usaini bila kusoma kwenye mstari bila kujua kimeandikwa Nini na jina la nani, sehemu nyingine hata jina halijaandikwa unaambiwa Saini hapa, na maafisa uchaguzi hawataki kuulizwa kwanini mmekata fedha, wanasema ndivyo ilivyo wao ndio wamesema wakati ni kinyume na tangazo la tumekaa time huru. Licha ya kuwepo TAKUKURU Nao wapo kimya huku wakishuhudia Haya. Pia tuna wasiwasi huenda Wana karatasi nyingine ambazo watasaini wao ofisini Kwa viwango vya time kwenye majina yetu

Lazima tume muwe na watu waadilifu, Kama wanaweza kuiba fedha ambazo ni stahiki ya mtu kufanya kazi, Je Imani inakuwa wapi ya watanzania Kwenye uchaguzi juu yenu.

Tusaidienu tupate stahiki zetu
 
Back
Top Bottom