Dhuluma inayotokana na kuaminiana: Nini kifanyike soma hii

Dhuluma inayotokana na kuaminiana: Nini kifanyike soma hii

Iziwari

Member
Joined
Jun 5, 2021
Posts
90
Reaction score
72
Dhuluma ni chanzo cha kwanza cha ugomvi na kutokuwa na maelewano kati ya watu wawili. Pia dhuluma yaweza kupelekea

Hata watu kutaftana na kutaka kuondoa uhai wa mwingine.

Cha hajabu kitendo cha kutaka kutoana uhai, hakimuathiri yule aliedhulumu tu. Bali kinamuathiri ata yule aliedhulumiwa.

Kitu ambacho ni hatari sana na kinahitaji kupata suluhisho la haraka kutokana na mawazo yetu wana jamii.

Labda niwape mfano ili kuelewa ninachokizungumza hapa.

Kuna siku kijana mmoja alikuwa anafanya kazi mgodini . Na ikafika mahali amepata mawe ya kutosha.

Kwa kipindi kirefu alikua anafanya kazi hiyo bila ya kupata matokeo, lakini sasa baada ya miaka kama minne ya kazi hiyo anakuja kupata matokeo. Yani anapata mawe yenye uwezo wa kumtajirisha.

Kijana huyu hakuwa amesoma sana. Kwamba alikua hajui kitu kuhusu soko la madini. Ikambidi aanze kuamini watu kwa kitu chochote wanachomwambia.

Kama inavosemekana kwenye msafara wa mamba na kenge wapo. Alikutana na kenge mmoja aliemuahidi kwamba akiuza madini yale nje ndio atapata faida kuliko kuyauza ndani.
Kijana mwenye yale madini akaamua kumuamini yule jamaa. Na wakaingia makubaliano ya kugawana kwa kiasi Fulani.

Kilichotokea baada ya hapo yule kenge aliamua kumtafuta yule kijana mwenye madini na kutaka kumuua na kujichukulia kila kitu mwenyewe.

Akatumia njia nyingi sana ikiwemo kumtumia wanawake na njia zingine mbaya Zaidi ila akashindwa.

Siku moja yule kijana mwenye madini yenye utajiri mkubwa akaja kugundua kwamba anawindwa na watu kutokana na kile alichonacho.

Ikawa akaenda mwenyewe kuyauza yale madini na kukimbia kabisa nchi.

Kitendo ambacho kiliwafanya watu wengi kukasirika sana na kusema bora asirudi maana tulikua na makubaliano naye.

Unaweza ukajiuliza nani hapo kadhulumiwa na nani ni mwenye haki.

Ukajua kwa urahisi tu mwenye haki. Lakini bado mwenye haki nae uhai wake ulikua matatani.

Dhuluma ni tatizo kubwa sana kwenye jamii zetu. Iwe imeshakutokea au iwe haijawahi kukutokea.

Watu wanapelekana mahakamani lakini bado wakitoka wameshikiana vinyongo.

Alieshinda na alieshindwa bado hawataki kukubali.

Kwaio bado hili swala ni gumu na linahitaji maarifa makubwa ya kulitatua.

Unaweza ukampa mtu mkopo kwa kumuamini akaja akataka na kutoa uhai wako pale unapoanza kumdai.

Somo ni kwamba usimwamini mtu. Bado watu ni kama Wanyama awe Tajiri au masikini.

Kwa upande wangu naweza nikasema kuna watu hawawezi kukuachia uwadhulumu. Watakutafuta tu mpaka wakupate. Na kuna watu wanaweza kusema wamemuachia mungu na mambo yakaisha.

Lakini kumbuka ukifika mahali unatamaa ya kudhulumu achana nayo. Na kama umeshadhulumiwa. Usichukue uamuzi wa hasira. Fanya maamuzi kwa utulivu na kwa mpangilio mzuri. Kama hautapata majibu uliokuwa unayategemea basi tafuta wazee wakushauri. Na songa mbele na Maisha yako.

Maana kuishi kwingi ni kuona mengi. Na hii dhuluma, wameshakutana nayo sana walioishi kwingi.

Achana kabisa na dhuluma uwe mtoto wa kike au wa kiume. Sio kitu chenye mwendelezo mzuri.
Toa maon yako hapo chini kama ulishawahi kupitia haya.
 
Ni jambo baya kudhulumu na haufiki mbali,maana si Haki yako!
 
DHulma inaharibu afya ya anayedhulumu na anayedhulimiwa pia asiposamehe.

Kuna namna seli za mwili huiga matendo yetu tunayofanyiana. Nadharia yangu hii.
 
Back
Top Bottom