Uchaguzi 2020 Dhuluma: Kitu pekee ambacho CCM wanategemea na kujivunia katika Uchaguzi huu

Uchaguzi 2020 Dhuluma: Kitu pekee ambacho CCM wanategemea na kujivunia katika Uchaguzi huu

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Sio Siri VIONGOZi na wanachama wa CCM mahala popote walipo huwa Kuna kitu wanajivuni kabla ya Uchaguzi. Hata kuwe na dalili za Uchaguzi kuwa mgumu namna gani CCM huwa hawana hofu. Na ndio maana mwaka huu wamejitokeza watia nia wengi sana kwa upande wa CCM kuliko chama chochote.

Kitu pekee inachojivunia CCM Ni dhuruma ya kura. Kwa kutumia nguvu za vyombo vya dola CCM huweza kudhulumu ushindi dhidi ya vyama vingine. Kila ukiongea, ama ukishindana kwa hoja na mwanaCCM juu ya Uchaguzi huu, ukimuambia muitikio wa watu kwenye mikutano ya Lissu mwanaCCM atakuambia yafuatayo:

Lissu hapati hata asilimia kumi. J, amejuaje wakati hata kura hazijapigwa? Na kura ni siri ya mtu?

Wengine wanakuambia, atuwezi kukabidhi nchi kwa wapinzani. Sasa najiuliza kama wananchi wakiamua nyinyi CCM ni nani hata kutokabidhi nchi wakati wananchi kwa uwingi wao wamemchagua?

Wengine hufikia hata kusema wapinzani hawatapata hata jimbo moja la ubunge. WanaCCM husema mengi. Lakini yote hayo ni kwa sababu wanategemea kuiba ushindi dhidi ya Upinzani.

Kitu pekee wanachotegemea ni Dhuluma. WanaCCM mkibisha kwa hili nawakumbusha Uchaguzi uliopita wa Serikali za mitaa mlidhulumu ushindi. Na safari hii hamna mnachokitegemea zaidi ya dhuluma, wizi na kupora ushindi.

Kwa mapokezi anayoyapata Lissu na kwa hoja anazozitoa Lissu ushindi wa kihalali kwenu hakuna kabisa. Mpaka hapo anayeongea ni Lissu pekee. Wapinzani wengine wakianza kuongea hamtapata la kuwajibu.
 
Chama dola wana mbinu nyingi sana za kushinda.
 
Leo idadi ya wapiga kura imetangazwa ni mil 29. Kiuhalisia watakaopiga kura ni mil 22, mil 7 ni reserve tutajazia pale tu zitakapohitajika. Tutapunguza mil 3 au NNE kujazia kwa mtu wetu ashinde.
 
CCM mwaka huu wagombea ubunge wengi walijitokeza ila ni mbinu imesukwa hata wao wenyewe bila kujua,lengo kubwa ni kurahisisha kukata majina ya watu kwenye kura za maoni ,wakiwa wachache inaleta attention ila kifo cha wengi hata waliowatarget wakiwakata lawama ni ndogo
 
Tuheshimiane tunajenga taifa moja, lolote lawezekana.Hongera Lissu, JPM na wengine.
 
Kwa namna vyama kongwe vya kiafrika vilivyo Ni vigumu kuondoka madarakani bila kumwaga damu angalau Zambia na Malawi kidogo walijtahidi.
 
CCM na serikali yake wametumia miaka hii karibia 5 sasa kwa umahiri wakutumikia Watanzania vizuri kwa juhudi na maarifa ya hali ya juu
Wamewajika mno kwa wananchi wengi wa hali za chini. Nidhamu na ufanisi kwenye ofisi za umma vimeimarika kwa kiwango cha kuridhisha.

CCM wanamtaji mkubwa sana kwa machinga, mama na baba lishe, bodaboda, wakulima, wafugaji, wachimbaji madini wadogo wadogo, nk. JPM na team yake serikalini na chamani wamekuwa watumishi wazuri wa Watanzania.

Kinacho takiwa ni kuunda team nzuri ya social mobilization basi. Na bahati wanazo raslimali watu na mali za uhakika na kutosha. Wakifanikiwa hilo umati utakaohudhuria kwenye kampemi za JPM sipati picha, watatakiwa kuchukua tahadhari za kiusalama kujiepusha maafa.
 
Kweli kabisa uyasemayo miaka mitano wametutumikia vzr sana ndio maana wakauziba mdomo upinzani usifurukute ili hata wakituteka huk MTAANI dunia isijue CCM oyeee
 
Mmewatia walimu umaskini mpaka wakistahafu wanaibiwa na kutapeliwa viinua mgongo kwasababu waliacha kadi za bank kwa wakopeshaji wa riba kubwa mitaani mwalimu akiingiziwa milioni Arobaini wakopeshaji waliochukua kadi yake wanakomba milioni 28 kila siku tunaona kwenye tv Leo mnajisifu mmewatumikia kwa weledi mkubwa mlaaniwe wahuni wakubwa nyie .
 
lee van cliff,

Dawa ya dhuluma ya kura na wizi wa kura Ni nguvu ya umma huwa haishindwi pooote duniani ,Algeria ,Sudan,Msri , Tunisia,kwa Likasheko huko ,sasa basi watanzania msitegee ushindi wa kura bila kuudai kwa nguvu ya umma, mjiandae kissikolojia daini ushindi wenu mwaka huuhuu Mpaka kieleweke ,mtu anayenufaika na madaraka huwa hayaachii kirashisi Mpaka alazimishwe, kama kweli watanzania wanataka ushindi wajiandae kwa nguvu ya umma hiyo ndio dawa pekee.
 
18 Julai 2020
Kibamba, Dar es Salaam
Tanzania

MAJIBIZANO MAKALI MSIMAMIZI WA UCHAGUZI NA MGOMBEA UBUNGE CHADEMA KIBAMBA/MSIMAMIZI AGOMA KUTOA FOMU



Maoni yangu:
Ofisi ya msimamizi wa uchaguzi hatoi ushirikiano ni kama kuna jambo limejificha, yaani Ofisi ya Msimamizi hajui jina, hawana picha, hawamjui kwa sura na malalamiko ya waliokuja kujitambulisha msimamizi kama mteule halali ofisi ya umma haitaki kutoa ushirikiano
 
lee van cliff,

Wengine husema hawawezi kukabidhi nchi kwa njia ya makaratasi. Wanasahau kumbe hata vyombo vya Dola vimeshasoma upepo. Vimeshaona wananvhi wanataka nini. Tusubiri october Lissu ataushangaza ulimwengu.
 
Back
Top Bottom