Mandesy
Senior Member
- Mar 22, 2018
- 115
- 125
Naandika ikiwa ni kuelezea masikitiko yangu dhidi ya ununuzi wa korosho kwa mwaka 2018/19.
Juzi tumetangatiwa kwamba kampuni ya Kenya itanunua tani laki moja ya korosho kwa shilingi bilioni 418. Kwa hesabu ya haraka haraka kampuni hiyo imenunua korosho ghafi kwa bei ya shilingi 4,180 kwa kilo. Hii ikulinganishwa na bei ya serikali ya shilingi 3,300 basi faida ghafi ni shilingi 880 kwa kilo na kwa kilo hizo zote zitakazonunuliwa na kampuni ya Kenya, yenye uhusiano ya Raila Odinga, Rafiki mkubwa wa JPM basi faida ni shilingi bilioni 88. Bado hujaondoa gharama za kukusanya na kusafirisha korosho.Taarifa za chinichini zinaonyesha kwamba hadi leo, serikali imelipa shilingi 2,600 kwa kilo ya korosho, ikiwa ni pungufu ya shilingi 700 kwa kilo kaw bei iliyotangazwa na wazalendo Mataga.
Wakati tani laki moja zikienda Kenya, bado kuna tani kama 130,000 aidha ziko mashambani ama kwenye maghala (warehose). Kati ya hizo inaonekana kwamba ni tani 80,000 tu ndizo zilizohakikiwa na kulipwa. Hii ina maana kwamba zaidi ya tani 150,000 zimechukuliwa kwa mabavu kwa kisingizio kwamba ni kangoma na wamiliki wake hawana uthibitisho kwamba korosho hizo ni zao. Hii inaonyesha kwamba serikali imezichukua hizo korosho bure na watatamba kwamba wamepata mabilioni ya fedha, kumbe ni dhuruma za watanzania;
Hii dhuluma imeambatana na kupigwa kwa watu na wengine kuhama nyumba zao wakiogopa kipigo cha polisi.
Ilitakiwa kwamba hadi kufikia jan 31, wakulima wote wame wamelipwa, lakini hadi leo ni robot u ya wakulima wameshalipwa, na wengine wanaambiwa korosho yao ni daraja la pili kwa hiyo hawatalipwa hiyo 3,300 kwa kilo.
Masikitiko ni kwamba serikali ilisema kwamba haitauza korosho ghafi nje ya nchi, lakini ushirika wa baba Raila Odinga na Mkulu, nepotism ya waziwazi imeanza kuonekana.
Leo serikali isitambe kwamba imeshighulikia suala la korosho, sio kweli, bali imefanya uporaji mkubwa sana ambao mamia ya watanzania wamekuwa maskini kutokana na kuporwa kwa mali zao.
MaiMai Worrier
Nanjilinji- Kilwa