Baada ya kunyakua tuzo
7 za KTMA 2014, na
kuwa nominated katika
tuzo za MTV MAMA
nchini Afrika Kusini,
sasa Diamond Platnumz ametajwa kuwania
tuzo kubwa zaidi za
kimataifa BET Awards
za nchini Marekani.
Hit single yake ya
Number 1 ndio
iliyompa tiketi Diamond
kuwa nominated katika
kipengele cha Best
International Act: Africa, ambapo
anachuana na mastaa
wengine wa Africa
ambao ni Davido
(Nigeria), Mafikizolo
(Afrika Kusini), Sarkodie (Ghana), na Tiwa Savage
(Nigeria). Diamond ndiye msanii
pekee wa Afrika
mashariki katika tuzo
hizo.
Hivi ndivyo
ilivyoandikwa katika
mtandao wa
www.bet.com BEST INTERNATIONAL
ACT: AFRICA NUMBER
ONE (TANZANIA)
TANZANIAN STAR
DIAMOND PLATNUMZ
BECAME A GLOBAL FORCE WITH SUCCESS OF HIS HIT
NUMBER ONE AND
THAT WAVE MAY
CONTINUE WITH A WIN
FOR BEST
INTERNATIONAL ACT: AFRICA.
Sherehe za ugawaji wa
tuzo hizo zitafanyika
June 29 huko Los
Angeles, Marekani
Tuzo za BET huandaliwa
na kituo cha TV cha
Black Entertainment
Television, na
zilianzishwa mwaka
2001 kusheherekea mafanikio ya kazi za
Wamarekani weusi
katika sanaa ya muziki,
uigizaji, michezo na
maeneo mengine ya
burudani. Hongera sana Diamond
Platnumz, endelea
kuipeperusha vizuri
bendera ya Tanzania.