Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,860
Msanii wa muziki wa Bongo Flavour kutoka Tanzania Diamond Platnumz.
Msanii wa muziki wa Bongo Flavour kutoka Tanzania Diamond Platnumz amekuwa akiongoza katika upigari kura wa kuwania tuzo za Muziki wa Televisheni ya Watu Weusi Marekani (Black Entertainment Television-BET) katika kipengele cha Best International Act: Africa.
Tuzo hizo zitatolewa jijini Los Angeles, Marekani Juni 29.
Mpaka jioni hii Diamond alikuwa anaongoza kwa asilimia 75.79.
Source BBC
Jamani kwenye tuzo za BET na tuzo nyingine za America hua mshindi hatafuti kwa kupigiwa kura na fans. Wao huwa wanautaratibu wa kuchagua baraza la watu 500 ambao hawa watu ndo wanapiga kura kwa kuchagua mshindi. Na kwa taarifa zilizopo ni kwamba Vanessa Mdee ni mmoja wa member kwenye hiyo kamati ambapo yeye anaiwakilisha Tanzania.
Hiyo link watu wanayopigia kura ni link ya mojawapo ya kituo cha radio kilichopo US amabcho hufanya hivo kuona watu wanamchagua nani na kamati imefanyaje maamuzi. Kura zinazopigwa kupitia hiyo link haziwezi saidia chochote kwenye kumpatia Diamond ushindi wa zile tuzo kama kamati haitampa kura.
BET wana-category huwa inadhaminiwa na Coca cola ambayo huitwa COCA COLA PEOPLE'S CHOICE AWARD ambayo kwa miaka kama mitatu mfululizo tuzo inachukuliwa na Chris Brown na hii ndo category pekee inayoruhusu watu kupiga kura, na pia hii sio category ambayo Our Beloved Son Diamond yupo.
So, najua tunatamani sana kumpigia kura Diamond ashinde but kwa wakati huu kura yetu haiweze kuleta effect yeyote, cha zaidi ni kuingia kwenye maombi mazito ili ile kamati ya watu 500 iweze kumwona Diamond-Platnumz na kumpatia ushind huu.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Diamond-Platnumz