Diamond afunga hospitali ya Amana kwa muda

Diamond afunga hospitali ya Amana kwa muda

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Mond.jpg

Mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amesherehekea siku yake ya kuzaliwa leo kwa kutembelea hospitali ya Amana ambako amesababisha shughuli zisimame kwa muda.

Katika ziara yake hiyo aliyoifanya leo Jumatatu, Diamond ametoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh4 milioni.

Muda wote aliokuwa hospitalini hapo wagonjwa na waliokuwa wakiwahudumia walitoka kwa ajili ya kumuona msanii huyo.

Diamond ambaye sasa anatamba na ngoma yake ya Hallelujah, amesema alifikia uamuzi wa kwenda kwenye hospitali hiyo kwa kuwa ndiyo mahali alipozaliwa.

Amesema anajivunia kuwa na watu wazuri wa karibu ambao wanamshauri kurudisha kwenye jamii inayomzunguka.

"Najua hospitali kuna mahitaji mengi nikaona kwa uwezo wangu mdogo nami nishiriki kusaidia mahali nilipozaliwa siku ya leo ili nipate pia fursa ya kuwaona watoto waliozaliwa tarehe kama yangu,"

"Nafahamu kuna changamoto nyingi, niwasihi watu wengine waangalie ni namna gani wanaweza kusaidia," amesema Diamond.

Kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo, Shaany Mwaruka amempongeza Diamond kwa uamuzi huo na kutaka watu wengine waige mfano huo.

"Ungeweza kusherehekea siku yako ya kuzaliwa kwa kufanya chochote kile, lakini ukakumbuka mahali ulipozaliwa."

Dk Mwaruka amesema hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba kutokana na idadi kubwa ya watu wanaowahudumia.

Kwenye ziara hiyo Diamond ameambatana na meneja wake, Said Fella.

Mwananchi
 
Good hata Mimi ni plan zangu hizi siku nikimuotea mhindi hata ka Milioni ntawatafuta wajitaji .... Mimi nimeokolewa hospital ya Mkoa ...pale SGD miaka ya 2002 mpaka nikachelewa kuanza shule ..... Nimeandikiwagwa barua kwa wino mwekundu ilikusudi niondoke pale Hosp.nikafie Nyumban lakin baba aligoma kawaambia Mimi naimani Mwanangu atapona na .... Hata akifa ninauwezo wa kumpeleka nyumbani .....dah .... Story ndefu acha tu .... Leo Niko fresh ....kwanini nikifanikiwa nisirudi kuwasupport ma dk wa sgd mkoani pale ... [emoji504][emoji490]
 
Tutatajirika kwa kile tukitoacho na si tukipokeacho... Vzr sana Chibu
 
Good hata Mimi ni plan zangu hizi siku nikimuotea mhindi hata ka Milioni ntawatafuta wajitaji .... Mimi nimeokolewa hospital ya Mkoa ...pale SGD miaka ya 2002 mpaka nikachelewa kuanza shule ..... Nimeandikiwagwa barua kwa wino mwekundu ilikusudi niondoke pale Hosp.nikafie Nyumban lakin baba aligoma kawaambia Mimi naimani Mwanangu atapona na .... Hata akifa ninauwezo wa kumpeleka nyumbani .....dah .... Story ndefu acha tu .... Leo Niko fresh ....kwanini nikifanikiwa nisirudi kuwasupport ma dk wa sgd mkoani pale ... [emoji504][emoji490]
Unataka uonewe huruma na mhindi.
 
Back
Top Bottom