Diamond afunga hospitali ya Amana kwa muda

Diamond afunga hospitali ya Amana kwa muda

Good hata Mimi ni plan zangu hizi siku nikimuotea mhindi hata ka Milioni ntawatafuta wajitaji .... Mimi nimeokolewa hospital ya Mkoa ...pale SGD miaka ya 2002 mpaka nikachelewa kuanza shule ..... Nimeandikiwagwa barua kwa wino mwekundu ilikusudi niondoke pale Hosp.nikafie Nyumban lakin baba aligoma kawaambia Mimi naimani Mwanangu atapona na .... Hata akifa ninauwezo wa kumpeleka nyumbani .....dah .... Story ndefu acha tu .... Leo Niko fresh ....kwanini nikifanikiwa nisirudi kuwasupport ma dk wa sgd mkoani pale ... [emoji504][emoji490]
Pole sana mkuu kwa machache uliyoandika umenigusa Long live Mkuu...
 
Good hata Mimi ni plan zangu hizi siku nikimuotea mhindi hata ka Milioni ntawatafuta wajitaji .... Mimi nimeokolewa hospital ya Mkoa ...pale SGD miaka ya 2002 mpaka nikachelewa kuanza shule ..... Nimeandikiwagwa barua kwa wino mwekundu ilikusudi niondoke pale Hosp.nikafie Nyumban lakin baba aligoma kawaambia Mimi naimani Mwanangu atapona na .... Hata akifa ninauwezo wa kumpeleka nyumbani .....dah .... Story ndefu acha tu .... Leo Niko fresh ....kwanini nikifanikiwa nisirudi kuwasupport ma dk wa sgd mkoani pale ... [emoji504][emoji490]
dah kweli kabisa mkuu unastori ya kipekee. sasa wengine tulizaliwa njiani wakati wanaelekea hosptali juu ya machela ya kijiji sijui turudishe shukrani wapi? yote na yote ni kumshukuru Mungu kutujalia uhai
 
Menej wake said fella?? Sio babu tale
 
Mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amesherehekea siku yake ya kuzaliwa leo kwa kutembelea hospitali ya Amana ambako amesababisha shughuli zisimame kwa muda.

Katika ziara yake hiyo aliyoifanya leo Jumatatu, Diamond ametoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh4 milioni.

Muda wote aliokuwa hospitalini hapo wagonjwa na waliokuwa wakiwahudumia walitoka kwa ajili ya kumuona msanii huyo.

Diamond ambaye sasa anatamba na ngoma yake ya Hallelujah, amesema alifikia uamuzi wa kwenda kwenye hospitali hiyo kwa kuwa ndiyo mahali alipozaliwa.

Amesema anajivunia kuwa na watu wazuri wa karibu ambao wanamshauri kurudisha kwenye jamii inayomzunguka.

"Najua hospitali kuna mahitaji mengi nikaona kwa uwezo wangu mdogo nami nishiriki kusaidia mahali nilipozaliwa siku ya leo ili nipate pia fursa ya kuwaona watoto waliozaliwa tarehe kama yangu,"

"Nafahamu kuna changamoto nyingi, niwasihi watu wengine waangalie ni namna gani wanaweza kusaidia," amesema Diamond.

Kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo, Shaany Mwaruka amempongeza Diamond kwa uamuzi huo na kutaka watu wengine waige mfano huo.

"Ungeweza kusherehekea siku yako ya kuzaliwa kwa kufanya chochote kile, lakini ukakumbuka mahali ulipozaliwa."

Dk Mwaruka amesema hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba kutokana na idadi kubwa ya watu wanaowahudumia.

Kwenye ziara hiyo Diamond ameambatana na meneja wake, Said Fella.

Mwananchi
Ya muhimu yanaachwa, pesa zinatumika kununua Madiwani.

Hongera Diamond
 
Kwa niaba ya team Kiba, tunampongeza Diamond pia, na sisi tutamwambia Kiba aige mazuri yote kutoka kwa Simba.
 
Kiba ashatoa misaada Amana, Muhimbili, Temeke, Mwananyala, na Chalinze lakini hapendi show off tu
kwani mashindano mkuu,hata huyo mondi hajafanya show off angeamua angejitangaza kabisa hata kwenye tv.....tusitake kila kitu tuweke mashindano jamani daaah
 
Ktk wana muziki wa kizazi kipya huyu kijana anafaa kupongezwa na jamii pamoja na viongozi wa kitaifa, vitu anavyofanya kwa jamii ni vitu vya maana, kama kutoa msaada Hosptali , kununua madawati 600. Kusaidia vituo vya watoto yatima , kuwa saidia vijana na kuwainua katika muziki , kuwapa ajira vijana kwa kuwa na wafanyakazi zaidi ya Hamsini , pia kutoa nafasi za vijana ambao wanauza karanga ambayo idadi yake inaanzia kiwandani , kwenye maduka ya jumla kwenye maduka ya mtaani na pia kwa machinga ambayo idadi yake tunaiona barabarani Hongera sana Daimondplutnumz
 
Kwa niaba ya team Kiba, tunampongeza Diamond pia, na sisi tutamwambia Kiba aige mazuri yote kutoka kwa Simba.
Ni wazo zuri mm nawapenda wana muzik wote lakini Kiba mbona hana moyo wa kusaidia wengine asiseme anatoa kimya kimya ukitoa kwa uwazi unawapa watu wengine mwamko wa kutoa hiyo kimya kimya anampa nani abadilike
 
Back
Top Bottom