Diamond afunguka kiroho mbaya kinachomfanya ampende Zari

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689
Wakati akihojiwa na Clouds Fm kipindi cha leo Tena alipoulizwa anachopenda zaidi kwa Zari ni kitu gani?

Alifunguka kuwa anachopenda ni tabia ya Zari ya kujielewa. Akaendelea kufunguka Zari anajua kutofautisha maisha yao halisi na maisha ya instagram. Kwani baada ya maisha ya instagram ya mapichapicha anajua kuwekeza kwa ajili ya kesho na ni mshauri wake wa mipango ya kimaendeleo.

Pia anasema anazimia ngozi yake Zari Ile mbaya.

Kasema mtarajie mtoto na atakuja kwenye social media kuwaomba mmchagulie Jina siku zikifika maana huyu ni mtoto wa kitaifa.

Amekataa katakata kusema kati ya Zari na Wema nani anayaweza zaidi licha ya kubananishwa sana na watangazaji.

Pia alitumia nafasi hiyo kukanusha uvumi kuwa kagombana na Fela baada ya kumshauri Fela awanunulie gari Yamoto kwani kasema Yamoto wanajengewa kila mtu nyumba yake kitu ambacho ni kikubwa kuliko gari. So huo uvumi ni wa uongo.

Pia alikanusha kuwa na nyama ya kusindika (beef) na Ommy Dimpoz.

Nb: Mimi nimependa hiyo spirit ya Zari muda wa kazi mnapiga kazi, muda wa mapenzi mapenzi na muda wa kuuza sura mnauza sura.
 
Yaani nyinyi mzae mtoto tena kwa njia za uzinzi uzinzi pasipo ndoa rasmi alafu mtuaminishe hapa kuwa atakuwa ni mtoto wa kitaifa, wajinga ndio waliwao!

Hapo sasa ndipo niliposhangaa! Watoto wa baba wa taifa tu hawajinadi ijekua yeye mjinga fulani?
Hizi sifa za kijinga ndizo zinazonifanya nisimkubali Diamond hata kidogo!
 
Hapo sasa ndipo niliposhangaa! Watoto wa baba wa taifa tu hawajinadi ijekua yeye mjinga fulani?
Hizi sifa za kijinga ndizo zinazonifanya nisimkubali Diamond hata kidogo!

Mtoto wa taifa hahahaa dah! Kweli ndomo ana furaha!
 
Hapo sasa ndipo niliposhangaa! Watoto wa baba wa taifa tu hawajinadi ijekua yeye mjinga fulani?
Hizi sifa za kijinga ndizo zinazonifanya nisimkubali Diamond hata kidogo!

Diamond ni msanii wa taifa so mie naona sawa mwanae kuwa mtoto wa taifa. Wala hakuna sifa za kijinga jamaa kaamua kuwa real.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…