Diamond akataa milioni mia tano za Lowassa

Duuh Hayo sio Maneno yangu Jamani , Gazeti la visa limeandika katika ukurasa wa mbele maneno hayo kama inavyoonyesha

Limeandika "Wakati wanamuziki wenzake wakilia njaa na kuoza kwa unga , Diamond akataa 500 Mil za Lowassa, Aambiwa ni Pesa Maalum kwa kazi Maalum na atakuwa Maalum 2015,
Naye Ajibu : Hizo Pesa peleka makanisani , misikitini ..Inatosha sana
 
Gazeti lenyewe linaitwa VISA..hivi huwa mnapata wapi muda wa kufatilia magazeti ya kiwaki kama haya!?
 
Kuna ushahidi wowote Lowassa alitaka kumpa pesa!
 
Haya bana yetu macho kwahiyo dogo hahongeki safi sana diamond umeonesha ukomavu na kutosheka.
 
hawezi kukataa pesa malaya kwa uzalenfo gani?kama anashindwa kuutunza uchi wake ataweza uutunza uzalendo wa taifa lake!!yule kama Dr.Slaa tu,imemshinda familia ya watu tano,ataweza watu milioni 45.
 
Huyi domo zege alikuwa ikulu juzi tu hapa tuna jua alichoambiwa atekeleze na baba riz 1,sk sio nyingi mtamuona kwenye majukwa ccm na suti za kijani,,!
 
Huyo angekuwa mwana CDM kaulimbiu yetu ni hii: KULA CCM lakini KURA CDM? Hizo pesa za wizi angezichukua tu na kuchangia CDM katika harakati za ukombozi na nyingine akaweka mfukoni kama halali yake.
 
Naona sasa wamedhamiria kuchafua nyota ya Diamond! Haya magazeti ya Shigongo ni shidaaa! Huyo Diamond amezikataa hizo fedha kwa vigezo gani? Kila siku anajituma kutengeneza fedha, eti leo akatae kisa zinatoka kwa Lowassa! Haiwezekani hata chembe! Hii mimi naichukulia kama muendelezo wa kumchafua lowassa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…