Diamond akiri kumpenda Omotola wa Nigeria

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
KING wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametengeneza kichwa cha habari nchini Nigeria baada ya kufunguka kuwa anampenda ‘vibaya’ staa wa filamu nchini humo, Omotola Jalade Ekeinde

Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond katika ziara ya kimuziki iitwayo ‘Nana Tour’ nchini humo, staa huyo ambaye kwa sasa ni mpenzi wa mjasiamali maarufu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amekuwa akiumizwa na penzi la Omotola kitambo sana lakini hakuwahi kuzungumza katika vyombo vya habari.

“Diamond ana maumbo yake flani hivi amazing ambayo huwa anayapenda, siku nyingi sana kabla hata hajakutana na Zari, alikuwa akituambia watu wake wa karibu kwamba miongoni mwa wanawake mastaa ambao anawatamani awaweke kwenye himaya ya penzi lake ni Omotola.

“Alisema anampenda kwa kila kitu kuanzia ufanyaji kazi wake, umbo lake na hata umaarufu mkubwa alionao ndani na nje ya Bara la Afrika,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya chanzo hicho kueleza habari hiyo, mapema wiki hii, mtandao wa nigeriafilms.com ulithibitisha maneno hayo kwa kuposti habari iliyobainisha Diamond anampenda Omotola sanjari na mastaa wengine wawili wa Nigeria anaovutiwa nao kimapenzi.

Akiwa hewani alipokuwa akihojiwa na redio moja jijini Lagos, Diamond aliweka bayana kuwa anateswa na penzi la mastaa watatu Nigeria, Omotola, Tonto Dikeh na Genevieve Nnaji.

“Jamaa kitambo sana anateswa na penzi la Omotola sasa leo kaongeza na wengine wawili na ninavyomjua hashindwi kufanya kweli ingawa nina wasiwasi kwa Omotola na Tonto maana wana waume zao labda ajiweke kwa Genevieve ambaye hajaolewa,” kilikazia chanzo chetu.

Diamond hakupatikana ili kusikia kauli yake juu ya ishu hiyo.

Chanzo: GPL
 

Attachments

  • 1435908613884.jpg
    92.9 KB · Views: 2,492
  • 1435908692857.jpg
    29.3 KB · Views: 2,341
Mmmh baba ubaya na wewe umezidi, tutaanza kukuita baba nisipitwe maana usione uchi unautaka mxiuuu, bahati mbaya mastaa wa nigeria wanajielewa na huyo omotola kaolewa na billionea sasa sijui utamdanganya na nini, au utampa murrano kimeo kama ya mama ubaya??
 
Kweli akili zetu waafrika ziko sehemu moja tu, jamaa anawaza pichu tu, ufuska mbaya sana
 

Heheh kumbuka hata zari nae alkuwa n mke wa bilionare tena na watoto wa3 ila jamaa akapenya.. Pia sioni diamond anamwacha vp zari naona bado yupo yupo nae sana.
 
Mwache awale tu, bado mdogo anakula ujana. Akikua atatulia.
 
Kwani KING wa Bongoflava ni huyu ama yule mwingine, au hii Tittle haina mwenyewe???
 
Huyu nae kiki mavi zitamuua

Hebu warumi tuletee ubuyu wa binti machozi
 
Last edited by a moderator:
Heheh kumbuka hata zari nae alkuwa n mke wa bilionare tena na watoto wa3 ila jamaa akapenya.. Pia sioni diamond anamwacha vp zari naona bado yupo yupo nae sana.

Zari alimfuata diamond kwa ajili ya umaarufu, zari alikuwa hajulikani kabla, so sasa hivi anapiga madil makubwa kupitia jina la diamond, omotola hawezi kumpata kirahisi, kamzidi ndomo umaarufu, elimu na pesa, yani awaache akina davido aende kwa ndomo kwa lipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…