Diamond alalamika baada ya show yake Ujerumani kuvurugika

fungi

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2014
Posts
2,539
Reaction score
4,672
Kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany.

Kinachoniuma na kunisikitisha zaidi ni jinsi watu walivyoamua kujitolea kuja kutusupport vijana wao kwa wingi, halafu mwisho wa s
iku promoter anatupeleka wasanii kwenye show saa kumi alfajiri.

Najua ni kiasi gani mmeumia na kuwa disappointed, Lakini naomba mtambue kuwa halikuwa ni kosa langu, coz mimi ni mgeni tu, na nafata maelekezo ya promoter, hivyo nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaoutaka mimi.

Haya ndio madhara ya ndugu zetu Mapromoter wa nje kutotaka kuamini na kukubali kuwa mziki wa East Africa sasa umekuwa, mwisho wa siku wanaandaa show kwenye venue ndogo halafu watu wanajaa hadi wanakosa pa kusimama na kuwabidi wapande kwa stage walau wapate pa kupumua.





====================================================================


 
Asante kwa taarifa..........lakini wala hakuna jipya kuchelewa kwenye show zake huyo kijana ndio zake,sijui ndio anaingia kwa mananzil....asiwachoshe wenzie...........
 
Diamond kwa level zake na mameneja kibao hawajui hata ratiba ya show? Unakwendaje kwenye show bila kujua ratiba? Alafu swala la muda ni kazi ya meneja kuhakikisha promota anaheshimu mkataba ambao muda ni sehemu yake.Yaani msanii mkubwa na meneja wako mnakaa tu hadi alfajiri ndio mnapelekwa ukumbini na nyie mnakwenda kama kuku tu.Diamond anastahili lawama na siku nyingine atambue lawama za msanii kuchelewa inaharibu zaidi jina la msanii si promota hivyo anapaswa kuhakikisha swala la promota kuheshimu muda linakuwa sehemu ya mkataba.
 
Hamna msanii hapa kazi kubana pua tu.ngoma ali kiba

Ameshaanza kutapatapa kuona mwenzie anafunika kwenye fiesta mikoani,yeye ile kill music ya kwao kigoma naskia aliwaboa watu pia
 
Pole ake mwaya
Ila shoo morning hyo kitu maajabu jaman ila hakuambiwa muda anaofanya shoo mapema maana izi kama komedy
 
huko hamna wazungu? naona ngozi nyeusi tu, halafu mbona ka grosary vile!

Wajerumani huwezi wakuta kwenye Show za vichochoroni, ukowakuta ni wale wala ndumu wanaokwenda kwa matazamio ya kupata ndumu toka kwa mablack... Dai awe makini, maana kila black Europe ni promoter, wana njaa hata fisi hafai. Mara nyingi wanawachelewesha wasanii ili wauze walau vinywaji kwanza.. Life tight jamaa
 
BONGE LA UKUMBI...kama madison square garden
 
suala ni kuwa ameona kapiga show uchochoron na kajuwa pics zitafika tz kaamua kujiwah et ukumbi hautosh
 
suala ni kuwa ameona kapiga show uchochoron na kajuwa pics zitafika tz kaamua kujiwah et ukumbi hautosh

Ha ha ha ha my ribs ile hapo padogo kama sebuleni mbona bora za fiesta unakuwa huru sasa msanii ana perfom huku watu wamemzingira wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…