fungi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,539
- 4,672
Kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany.
Kinachoniuma na kunisikitisha zaidi ni jinsi watu walivyoamua kujitolea kuja kutusupport vijana wao kwa wingi, halafu mwisho wa siku promoter anatupeleka wasanii kwenye show saa kumi alfajiri.
Najua ni kiasi gani mmeumia na kuwa disappointed, Lakini naomba mtambue kuwa halikuwa ni kosa langu, coz mimi ni mgeni tu, na nafata maelekezo ya promoter, hivyo nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaoutaka mimi.
Haya ndio madhara ya ndugu zetu Mapromoter wa nje kutotaka kuamini na kukubali kuwa mziki wa East Africa sasa umekuwa, mwisho wa siku wanaandaa show kwenye venue ndogo halafu watu wanajaa hadi wanakosa pa kusimama na kuwabidi wapande kwa stage walau wapate pa kupumua.
====================================================================

Watu kadhaa wamejeruhiwa mjini Stuttgart baada ya kutokea vurugu zilizotokana na kushindwa kufanya onyesho lake la Jumamosi ya Agosti 30, mwanamzuki wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnum. Mwamamuziki huyo aliefika katika ukumbi alfajiri ya kuamkia Jumapili aliokolewa na polisi kutoka katika mikono ya mashabiki wenye hasira. Onyesho hili liliandaliwa na kampuni ya Kinaijeria iitwayo Brotes Events kwa kushirikiana na watanzania kadhaa wa hapa Ujerumani.
Chanzo: DW
=============================================
![]()
Gari ya Polisi iliyoibuka kumuokoa Diamond kufuatia sakata la mashabiki wake kupandwa na jazba
Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini stuttgart,ujerumani
Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe 30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake,Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.
Mmoja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ Flor alipatwa shock mshtuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospatal.
Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND"
source:stuttgarter-nachrichten.de
my take: Muda ni kitu Muhimu