Diamond alalamika baada ya show yake Ujerumani kuvurugika

m_kishuri kweli mkuu ulaya wazungu kama umeenda ulaya ukapiga picha lakn katika iyo picha kama hatujamwona mdhugu wewe hukwenda ulaya kamba tu, labda uliificha zako makambako !
 
suala ni kuwa ameona kapiga show uchochoron na kajuwa pics zitafika tz kaamua kujiwah et ukumbi hautosh

Inawezekana Mkuu..Maana Show yake Malaysia nayo Alifanya alfajiri..Na ukumbi ulikuwa Mdogo..Show pia ilikuwa Mbaya..Ajabu sikuona kuzungumzia hilo..Sasa limejirudia..

Ajitahidi kurekebisha hilo..Kabla hayajamkuta..
 
Siku hzi mnafanya show grossary? mwanzo mlikuwa mnafanya sebuleni hongereni kwa ku-advance.
Hamna bhana, ukumbi ni mkubwa kishenzi lakini sio ukumbi wa muziki...dizaini kama PTA Hall pale Uwanja wa Sabasaba!!!
 
Watu kadhaa wamejeruhiwa mjini Stuttgart baada ya kutokea vurugu zilizotokana na kushindwa kufanya onyesho lake la Jumamosi ya Agosti 30, mwanamzuki wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnum. Mwamamuziki huyo aliefika katika ukumbi alfajiri ya kuamkia Jumapili aliokolewa na polisi kutoka katika mikono ya mashabiki wenye hasira. Onyesho hili liliandaliwa na kampuni ya Kinaijeria iitwayo Brotes Events kwa kushirikiana na watanzania kadhaa wa hapa Ujerumani.

Chanzo: DW
=============================================





Gari ya Polisi iliyoibuka kumuokoa Diamond kufuatia sakata la mashabiki wake kupandwa na jazba







Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini stuttgart,ujerumani

Stuttgart,Ujerumani,

Usiku wa Jumamosi ya Tarehe 30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake,Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.

Mmoja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ Flor alipatwa shock mshtuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospatal.

Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND"

source:stuttgarter-nachrichten.de



my take: Muda ni kitu Muhimu
 
Sasa yule babu tale kazi yake nini kama manager,coz ni lazima uone ukumbi, ujue time na malipo then ufunge mkataba, yawezekana mikataba yao wanafungia kwenye computer ,kwa email negotiation na picture

shule ni tatizo kwa babu tale.
 
[h=1]POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA ![/h]

KAFIKA UKUMBINI SAA 10 ALFAJIRI ! WASHABIKI WANASURI SHOW TANGU SAA 4 USIKU

PROMOTA MNAIJERIA AINGIA MITINI ,DJ APATA KISAGO HETI VYOMBO VIBOVU ! HAIBU

Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe 30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.


Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake,

Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki
ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.moja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la haibu alijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa
wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.


Source:Blaulicht aus der Region Stuttgart: 31. August: Diamond Platnumz zieht Ärger der Fans auf sich - Region - Stuttgarter Nachrichten
 
Huyu si ndiye kapigiwa ndogondogo na nanii hivi karibuni? mie nilidhani ubabaishaji unafanywa hapa bongo kwakuwa wabongo wamezoea kudanganywa, hii aibu ubabaishaji mpaka ughaibuni!! partnership na m-nigeria?!!! hawa si ndiyo usiku kucha wanatapeli watu kwenye mitandao?! ama kweli bora ya Musa yana nafuu.
 
yule jamaa design kama kalewa sifa za kijinga, pia mleta mada unatakiwa udhibitishe habari yako kwa picha na chanzo.
 
Sio tatizo lake ni promota

Go go go Diamond Gooo
 
idoyo

Eheee!!!hivi hao waandaji hawajui kuwa kitu TIME ni rasilimali kuu ya kuzingatia kwa wenzetu?Hakuna uswahili swahili huko kuhusu muda,ukitaka kukosana na wazungu wazingue kuhusu muda mliopatana kutekeleza jambo,WAJERUMANI ndo usichezee kitu kinaitwa MUDA,watakutoa ngeu za chupa si za ngumi.Poleni sana,kwani kutembea ndio kujifunza:hail:
 
Last edited by a moderator:
ACHA UONGO . Ati anusurika kipigo!! Yeye alipelekwa kwenye Show late hivyo mashabiki wakahamaki na kuvuruga ukumbi, na hata hakuguswa, kafika mapolisi tayari wakiwa wameshadhibiti.
 
yule jamaa design kama kalewa sifa za kijinga, pia mleta mada unatakiwa udhibitishe habari yako kwa picha na chanzo.

picha, chanzo. vyote vipo hapo
 
Chezea huku Ughaibuni, watu hata wakiwa kanisani wanaangalia muda !!!
 
Picha zinaeleza kila kitu,mtiti unaonekana ulikuwa mzito na si wa kitoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…